Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Isaya 56:3-7

Isaya 56:3-7 BHN

“Mgeni anayenitambua mimi Mwenyezi-Mungu asifikiri: ‘Hakika Mwenyezi-Mungu atanitenga na watu wake.’ Naye towashi asiseme: ‘Mimi ni mti mkavu tu!’ Maana mimi Mwenyezi-Mungu nasema: Towashi ashikaye sheria zangu za Sabato, anayefanya mambo yanayonipendeza, na kulizingatia agano langu, nitampa nafasi maalumu na ya sifa katika nyumba yangu na kuta zake; nafasi bora kuliko kuwa na watoto wa kiume na wa kike: Nitampa jina la kukumbukwa daima, na ambalo halitafutwa kamwe. “Watu wageni watakaonikiri mimi Mwenyezi-Mungu, watakaoniheshimu, wakapenda jina langu na kuwa watumishi wangu, wote watakaoshika Sabato bila kuikufuru, watu watakaozingatia agano langu, hao nitawaleta katika mlima wangu mtakatifu, na kuwafurahisha katika nyumba yangu ya sala; tambiko na sadaka zao zitakubaliwa madhabahuni pangu. Maana nyumba yangu itaitwa: ‘Nyumba ya sala kwa ajili ya watu wote’.

Soma Isaya 56