Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Isaya 49:1-7

Isaya 49:1-7 BHN

Nisikilizeni, enyi nchi za mbali, tegeni sikio, enyi watu wa mbali! Mwenyezi-Mungu aliniita kabla sijazaliwa, alitaja jina langu nikiwa tumboni mwa mama yangu. Aliyapa ukali maneno yangu kama upanga mkali, alinificha katika kivuli cha mkono wake; aliufanya ujumbe wangu mkali kama ncha ya mshale, akanificha katika podo lake. Aliniambia, “Wewe ni mtumishi wangu; kwako, Israeli, watu watanitukuza.” Lakini mimi nikafikiri, “Nimeshughulika bure, nimetumia nguvu zangu bure kabisa.” Hata hivyo, Mwenyezi-Mungu atanipa haki yangu; tuzo la kazi yangu liko kwa Mungu. Lakini asema sasa Mwenyezi-Mungu, ambaye aliniita tangu tumboni mwa mama yangu ili nipate kuwa mtumishi wake; nilirudishe taifa la Yakobo kwake, niwakusanye wazawa wa Israeli kwake. Mwenyezi-Mungu amenijalia heshima mbele yake. Mungu wangu amekuwa ndiye nguvu yangu. Yeye asema: “Haitoshi tu wewe kuwa mtumishi wangu, uyainue makabila ya Yakobo, na kurekebisha watu wa Israeli waliobaki. Nitakufanya uwe mwanga wa mataifa, niwaletee wokovu watu wote duniani.” Mwenyezi-Mungu, Mkombozi na Mtakatifu wa Israeli, amwambia hivi yule anayedharauliwa mno, yule anayechukiwa na mataifa, na ambaye ni mtumishi wa watawala: “Wafalme watakuona nao watasimama kwa heshima, naam, wakuu watainama na kukusujudia kwa sababu yangu mimi Mwenyezi-Mungu ambaye hutimiza ahadi zangu; kwa sababu yangu mimi Mtakatifu wa Israeli ambaye nimekuteua wewe.”

Soma Isaya 49