Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Isaya 49:1-7

Isaya 49:1-7 NENO

Nisikilizeni, enyi visiwa, sikieni hili, ninyi mataifa mlio mbali: Kabla sijazaliwa, BWANA aliniita, tangu kuzaliwa kwangu, amelitaja jina langu. Akafanya kinywa changu kuwa kama upanga ulionolewa, katika uvuli wa mkono wake akanificha; akanifanya kuwa mshale uliosuguliwa, na kunificha katika podo lake. Akaniambia, “Wewe u mtumishi wangu, Israeli, ambaye ndani yake nitaonesha utukufu wangu.” Lakini nilisema, “Nimetumika bure, nimetumia nguvu zangu bure bila faida. Hata hivyo linalonistahili liko mkononi mwa BWANA, nao ujira wangu uko kwa Mungu wangu.” Sasa BWANA asema: yeye aliyeniumba tumboni kuwa mtumishi wake, kumrudisha tena Yakobo kwake na kumkusanyia Israeli, kwa maana nimepata heshima machoni pa BWANA, naye Mungu wangu amekuwa nguvu yangu; yeye asema: “Je, ni jambo dogo sana wewe kuwa mtumishi wangu ili kurejesha makabila ya Yakobo, na kuwarudisha wale Waisraeli niliowahifadhi? Pia nitakufanya uwe nuru kwa ajili ya watu wa Mataifa, ili upate kuleta wokovu wangu hata miisho ya dunia.” Hili ndilo asemalo BWANA, yeye Mkombozi na Aliye Mtakatifu wa Israeli, kwake yeye aliyedharauliwa na kuchukiwa na taifa, kwa mtumishi wa watawala: “Wafalme watakuona na kusimama, wakuu wataona na kuanguka kifudifudi, kwa sababu ya BWANA, aliye mwaminifu, yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli, aliyekuchagua wewe.”