Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 Samueli UTANGULIZI

UTANGULIZI
Chanzo cha kitabu hiki cha pili cha Samueli ni kile cha kwanza. Hiki na kile cha kwanza hufanya kitu kimoja na hiki kinaendelea na habari pale zilipoachiwa katika kitabu cha kwanza. Katika kitabu hiki tunapewa habari za mfalme Daudi, kwanza kama mtawala wa Yuda, yaani sehemu ya kusini ya nchi hiyo, kisha kama mtawala wa nchi yote ya Israeli. Daudi anaoneshwa kuwa mtu wa imani kubwa na mwenye kumtegemea Mungu kwa moyo. Hata hivyo, tunaoneshwa kwamba alikuwa pia mtu ambaye hakuwa na huruma tena karibu mkatili na ambaye alikuwa hata tayari kutenda dhambi mbaya sana ili kujinufaisha yeye mwenyewe. Lakini anapokumbana na dhambi zake mwenyewe, kwa mfano wakati nabii Nathani alipomkabili, Daudi anaungama na kukiri makosa yake na kupokea adhabu anayostahili kutoka kwa Mungu. Maisha ya Daudi na mambo aliyoyatenda yaliacha kumbukumbu thabiti katika mioyo ya Waisraeli. Kwa hiyo, Waisraeli walipokumbana na taabu baadaye walitamani kumpata mfalme wa namna ya Daudi; mwana wa Daudi; yaani wa ukoo wa Daudi; ambaye angekuwa kama yeye.

Iliyochaguliwa sasa

2 Samueli UTANGULIZI: BHN

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha