Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 Petro UTANGULIZI

UTANGULIZI
Walioandikiwa barua hii ni Wakristo kwa jumla, wote waliojaliwa imani ileile aliyojaliwa mwandishi na wenzake (1:1).
Lengo la mwandishi ni kupinga mafundisho ya watu fulani ambayo yalipingana na ukweli wa Habari Njema. Njia moja maalumu ya kuwakabili watu hao waliojipenyeza katika jumuiya ya kanisa ni kwa waumini kuishi na kuzingatia mafundisho ya kweli juu ya kumjua Mungu na Mwanawe Yesu Kristo kama yalivyopokelewa na wale waliomwona Yesu Kristo kwa macho yao wenyewe na kusikiliza aliyoyafundisha.
Mwandishi ambaye anajitaja kama “Simoni Petro, mtumishi na mtume wa Yesu Kristo” (1:1), anajitangaza kuwa shahidi wa kugeuka sura kwa Bwana (1:16-18) na mwandishi wa barua moja iliyotangulia hii (3:1) na bila shaka ndiye mtume Petro.
Yaliyomo na muundo wa barua hii
Kwanza, mwandishi ana salamu (1:1-2). Pia maneno au mwito kwa waumini wafikirie zile ahadi kuu na za thamani kubwa walizopewa na Mungu kuhusu kuishiriki hali yake Mungu (1:4). Mwandishi anatilia mkazo tangu mwanzo wa barua hii, mambo ya lazima yanayohusu maisha ya Kikristo na juu ya kuwa waaminifu kwa mwito wa Mungu kulingana na yale yanayotangazwa na kufundishwa na wale watu waliomwona Bwana Yesu.
Katika sura ya 2:1-22 mwandishi anashutumu kwa nguvu shughuli na tabia ya hao waalimu wa uongo waliokuwa wanaeneza mafundisho ya uongo.
Katika sura ya 3 tunagundua kwamba watu hao walikuwa hasa wakiwazomea wale waumini waliokuwa wanangojea kurudi kwake Kristo na kuwaambia ati jambo hilo halitatukia. Mwandishi anajibu kwa kusisitiza kwamba kuchelewa huko ni kwa sababu Mungu ni mvumilivu; anapenda kusubiri zaidi ili watu wengi zaidi wapate fursa ya kukubali kuokolewa.

Iliyochaguliwa sasa

2 Petro UTANGULIZI: BHN

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha