Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zakaria 2

2
Mtu ashikaye kamba ya kupimia.
1Nilipoyainua macho yangu, nichungulie, mara nikaona mtu, naye alishika mkononi mwake kamba ya kupimia.#Ez. 40:3. 2Nikamwuliza: Unakwenda wapi? Akaniambia: Ninakwenda kuupima Yerusalemu, nione, upana wake na urefu wake ulivyo. 3Mara malaika aliyesema na mimi akatoka, kisha malaika mwingine akatokea kukutana naye, 4akamwambia: Piga mbio, umwambie yule kijana kwamba: Yerusalemu utakaa watu pasipo boma kwa wingi wa watu na nyama watakaokuwamo mwake.#Ez. 38:11. 5Kisha mimi nitakuwa boma la moto litakalouzunguka nao utukufu wake uliomo mwake utakuwa mimi; ndivyo, asemavyo Bwana.#Zak. 9:8.
Siku za furaha za kurudi toka Babeli.
6Ndivyo, asemavyo Bwana: Haya! Haya! Kimbieni, mwitoke nchi hiyo ya kaskazini! Kwani nimewatawanya ninyi katika pande zote nne za upepo wa angani; ndivyo, asemavyo Bwana. 7Haya! Jiponye, Sioni ukaaye kwake binti Babeli! 8Kwani hivi ndivyo, Bwana Mwenye vikosi anavyosema: Kuutokeza utukufu amenituma kwa wamizimu walioziteka mali zenu ninyi, kwani anayewagusa ninyi huigusa mboni ya jicho lake.#5 Mose 32:10. 9Ndipo, mtakaponiona, nikiwapungia kwa mkono wangu; ndipo, wao watakapokuwa mateka yao walio watumwa wao, mpate kujua, ya kuwa Bwana Mwenye vikosi amenituma.
Wamizimu nao watamgeukia Bwana.
10Shangilia kwa furaha, binti Sioni! Kwani utaniona, nikija kukaa katikati yako; ndivyo, asemavyo Bwana. 11Siku hiyo itakuwa, wamizimu wengi waje kuandamana na Bwana; ndipo, wao nao watakapokuwa ukoo wangu. Nitakaa katikati yako, upate kujua, ya kuwa Bwana Mwenye vikosi amenituma kwako.#Yes. 11:10. 12Ndipo, Bwana atakapowatwaa Wayuda, wawe fungu lake katika nchi hii takatifu, nao Yerusalemu atauchagua tena, uwe mji wake.#Zak. 1:17. 13Wote wenye miili ya kimtu sharti wanyamaze kimya usoni pake Bwana, kwani amekwisha kuondoka katika Kao lake takatifu!#Hab. 2:20.

Iliyochaguliwa sasa

Zakaria 2: SRB37

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia