Wafilipi 2:9-11
Wafilipi 2:9-11 TKU
Hivyo ndiyo sababu Mungu alimpa mahali pa heshima sana, na akampa jina lililo kuu kuliko majina yote. Hivyo kila mtu atasujudu kumheshimu Yesu. Kila mmoja aliye mbinguni, duniani na wale walio chini ya dunia. Wote watakiri kwamba, “Yesu Kristo ni Bwana,” na hili litamtukuza Mungu Baba.