Esta 10
10
Ukuu wa Ahasuero na Mordekai
1Mfalme Ahasuero alitoza kodi watu wa bara na pwani. 2Matendo yake yote makuu na ya ajabu, pamoja na simulizi kamili kuhusu jinsi alivyompandisha cheo Mordekai na kumtunukia heshima kuu, yote yameandikwa katika Kitabu cha Kumbukumbu za wafalme wa Media na Persia.#10:2 Kitabu cha Kumbukumbu za Wafalme wa Media na Persia: Kitabu cha namna hiyo hakijulikani au hakikuhifadhiwa. 3Mordekai, Myahudi, alikuwa wa kwanza chini ya mfalme Ahasuero katika madaraka. Alipendwa na kuheshimiwa na Wayahudi, maana aliwafanyia mema watu wake na kuwatakia amani wazawa wao wote.
Iliyochaguliwa sasa
Esta 10: BHNTLK
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Copyright The Bible Society of Tanzania, 1993
The Bible Society of Kenya 1993