Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Warumi 4

4
Mfano wa Abrahamu
1Basi, tusemeje juu ya Abrahamu, baba yetu kwa jinsi ya mwili? 2Kwa maana ikiwa Abrahamu alihesabiwa haki kwa ajili ya matendo yake, analo la kujisifia; lakini si mbele za Mungu. 3#Mwa 15:6; Gal 3:6; Yak 2:23 Maana Maandiko yasemaje? Abrahamu alimwamini Mungu, ikahesabiwa kwake kuwa haki. 4#Rum 11:6; Mt 20:7,14 Lakini kwa mtu afanyaye kazi, ujira wake hauhesabiwi kuwa ni neema, bali kuwa ni deni. 5Lakini kwa mtu asiyefanya kazi, bali anamwamini yeye ambaye amhesabia haki asiyekuwa mtauwa, imani yake mtu huyo imehesabiwa kuwa haki. 6#Zab 32:1,2 Kama vile Daudi ainenavyo heri yake mtu yule ambaye Mungu amhesabia kuwa na haki pasipo matendo,
7 # Zab 32:1-2 Heri waliosamehewa makosa yao,
Na waliositiriwa dhambi zao.
8Heri mtu yule ambaye Bwana hamhesabii dhambi.
9 # Mwa 15:6 Basi je! Heri hiyo ni kwa hao waliotahiriwa, au kwa hao pia wasiotahiriwa? Kwa kuwa tunanena ya kwamba kwake Abrahamu imani yake ilihesabiwa kuwa ni haki. 10Alihesabiwaje basi? Alipokwisha kutahiriwa, au kabla hajatahiriwa? Si baada ya kutahiriwa, bali kabla ya kutahiriwa. 11#Mwa 17:10,11 Naye aliipokea dalili hii ya kutahiriwa, mhuri wa ile haki ya imani aliyokuwa nayo kabla hajatahiriwa; apate kuwa baba yao wote waaminio, ijapokuwa hawakutahiriwa, ili na wao pia wahesabiwe haki; 12#Mt 3:9; 1 Pet 2:21; 2 Kor 12:18 tena awe baba ya kutahiriwa, kwa wale ambao si waliotahiriwa tu, bali pia wanazifuata nyayo za imani yake baba yetu Abrahamu aliyokuwa nayo kabla hajatahiriwa.
Ahadi ya Mungu yatimizwa kwa imani
13 # Mwa 17:4-6; 22:17-18; Gal 3:29 Kwa maana ahadi ile ya kwamba atakuwa mrithi wa ulimwengu alipewa Abrahamu na uzao wake, si kwa sheria bali kwa haki aliyohesabiwa kwa imani. 14#Gal 3:18 Maana ikiwa wale wa sheria ndio warithi, imani imekuwa bure, na ahadi imebatilika. 15#Rum 3:20; 5:13; 7:8,10 Kwa sababu sheria ndiyo ifanyayo hasira; maana pasipokuwapo sheria, hapana kosa. 16#Gal 3:7 Kwa hiyo ilitoka katika imani, iwe kwa njia ya neema, ili kwamba ile ahadi iwe imara kwa wazawa wote; si kwa wale wa torati tu, ila na kwa wale wa imani ya Abrahamu; aliye baba yetu sisi sote; 17#Mwa 17:5; Isa 48:13 (kama ilivyoandikwa, Nimekuweka kuwa baba wa mataifa mengi); mbele zake yeye aliyemwamini, yaani Mungu, mwenye kuwahuisha wafu, ayatajaye yale yasiyokuwako kana kwamba yamekuwako. 18#Mwa 15:5 Naye aliamini kwa kutarajia yasiyoweza kutarajiwa, ili apate kuwa baba wa mataifa mengi, kama ilivyonenwa, Ndivyo utakavyokuwa uzao wako. 19#Mwa 17:17 Yeye asiyekuwa dhaifu wa imani, alifikiri hali ya mwili wake uliokuwa umekwisha kufa, (akiwa amekwisha kupata umri wa kama miaka mia moja), na hali ya utasa wa tumbo lake Sara.#4:19 Katika Kigiriki ni ‘hali ya kufa ya tumbo lake Sara’. 20#Ebr 11:7,11,34 Lakini akiiona ahadi ya Mungu hakusita kwa kutoamini, bali alitiwa nguvu kwa imani, akimtukuza Mungu; 21huku akijua hakika ya kuwa Mungu aweza kufanya yale aliyoahidi. 22#Mwa 15:6 Kwa hiyo ilihesabiwa kwake kuwa ni haki. 23#Rum 15:4 Lakini haikuandikwa kwa ajili yake tu kwamba ilihesabiwa kwake; 24#1 Pet 1:21 bali na kwa ajili yetu sisi mtakaohesabiwa vivyo hivyo, sisi tunaomwamini yeye aliyemfufua Yesu Bwana wetu katika wafu; 25#Isa 53:4-5; 1 Kor 15:17 ambaye alitolewa kwa ajili ya makosa yetu, na kufufuliwa ili mpate kuhesabiwa haki.

Iliyochaguliwa sasa

Warumi 4: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha