Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Warumi 11

11
Kukataliwa kwa Israeli hakutadumu
1 # Flp 3:5; Zab 94:14; 1 Sam 12:22; Yer 31:37 Basi, nauliza, Je! Mungu aliwasukumia mbali watu wake? La hasha! Kwa kuwa mimi nami ni Mwisraeli, mmoja wa wazawa wa Abrahamu, mtu wa kabila la Benyamini. 2#1 Fal 19:10,14 Mungu hakuwasukumia mbali watu wake aliowajua tokea awali. Au hamjui yale yaliyonenwa na Maandiko juu ya Eliya? Jinsi anavyowashitaki Waisraeli mbele za Mungu, 3#1 Fal 19:10,14 Bwana, wamewaua manabii wako, wamezibomoa madhabahu zako, nami nimebaki peke yangu, nao wananitafuta roho yangu. 4#1 Fal 19:18 Lakini lile jibu la Mungu lamwambiaje? Nimejibakizia watu elfu saba wasiopiga goti mbele ya Baali. 5#Rum 9:27 Basi ni vivi hivi wakati huu wa sasa, yako mabaki waliochaguliwa kwa neema. 6#Gal 3:18 Lakini ikiwa ni kwa neema, haiwi kwa matendo tena, au hapo neema isingekuwa neema. 7#Rum 9:31 Imekuwaje basi? Kitu kile ambacho Israeli alikuwa akikitafuta hakukipata; lakini wale waliochaguliwa walikipata, na wengine walitiwa ugumu. 8#Kum 29:4; Isa 29:10 Kama ilivyoandikwa, Mungu aliwapa roho ya usingizi, macho hata wasione, na masikio hata wasisikie, hata siku hii ya leo. 9#Zab 69:22-23; 35:8 Na Daudi asema,
Meza yao na iwe tanzi na mtego,
Na kitu cha kuwakwaza, na malipo kwao;
10Macho yao yatiwe giza ili wasione,
Ukawainamishe mgongo wao siku zote.
Kuokolewa kwa mataifa
11 # Kum 32:21; Mdo 13:46; Rum 10:19 Basi nasema, Je! Wamejikwaa hata waanguke kabisa? La hasha! Lakini kwa kosa lao wokovu umewafikia Mataifa, ili wao wenyewe watiwe wivu. 12Basi, ikiwa kosa lao limekuwa utajiri wa ulimwengu, na upungufu wao umekuwa utajiri wa Mataifa, je! Si zaidi sana utimilifu wao?
13Lakini nasema na ninyi, mlio watu wa Mataifa. Basi, kwa kadiri nilivyo mtume wa watu wa Mataifa, naitukuza huduma iliyo yangu, 14#1 Tim 4:16 nipate kuwatia wivu walio damu moja na mimi na kuwaokoa baadhi yao. 15Maana ikiwa kutupwa kwao kumeleta upatanisho kwa ulimwengu, je! Kukubaliwa kwao kutakuwa nini kama si uhai baada ya kufa? 16#Hes 15:17-21 Tena malimbuko yakiwa matakatifu, kadhalika na donge lote; na shina likiwa takatifu, matawi nayo kadhalika. 17#Efe 2:11-19 Lakini iwapo matawi mengine yamekatwa, na wewe mzeituni mwitu ulipandikizwa kati yao, ukawa mshirika wa shina la mzeituni na unono wake, 18#Yn 4:22 usijisifu juu ya matawi yale; au ikiwa wajisifu, si wewe ulichukuaye shina, bali ni shina likuchukualo wewe. 19Basi utasema, Matawi yale yalikatwa kusudi ili nipandikizwe mimi. 20#Rum 12:16 Vema. Yalikatwa kwa kutoamini kwao, na wewe wasimama kwa imani yako. Usijivune, bali uogope. 21Kwa maana ikiwa Mungu hakuyaachia matawi ya asili, wala hatakuachia wewe. 22#Yn 15:2,4; Ebr 3:14 Tazama, basi, wema na ukali wa Mungu; kwa wale walioanguka, ukali, bali kwako wewe wema wa Mungu, ukikaa katika wema huo; kama sivyo, wewe nawe utakatiliwa mbali. 23#2 Kor 3:16 Na hao pia, wasipokaa katika kutoamini kwao, watapandikizwa; kwa kuwa Mungu aweza kuwapandikiza tena. 24Kwa maana ikiwa wewe ulikatwa ukatolewa katika mzeituni, ulio mzeituni mwitu kwa asili yake, kisha ukapandikizwa, kinyume cha asili, katika mzeituni ulio mwema, si zaidi sana wale walio wa asili kuweza kupandikizwa katika mzeituni wao wenyewe?
Israeli wote wataokolewa
25 # Lk 21:24; Yn 10:16; Rum 12:16 Kwa maana, ndugu zangu, sipendi msiijue siri hii, ili msijione kuwa wenye akili; ya kwamba kwa sehemu ugumu umewapata Israeli, mpaka utimilifu wa Mataifa uwasili. 26#Isa 59:20; 27:9; Mt 23:39; Zab 14:7 Hivyo Israeli wote wataokoka; kama ilivyoandikwa,
Mwokozi atakuja kutoka Sayuni;
Atamtenga Yakobo na maasia yake.
27 # Yer 31:33-34; Isa 27:9 Na hili ndilo agano langu nao,
Nitakapowaondolea dhambi zao.
28Basi kwa habari ya Injili wamekuwa adui kwa ajili yenu; bali kwa habari ya kule kuchaguliwa wamekuwa wapenzi kwa ajili ya baba zetu. 29Kwa sababu karama za Mungu hazina majuto, wala mwito wake. 30Kwa maana kama ninyi zamani mlivyomwasi Mungu, lakini sasa mmepata rehema kwa kuasi kwao; 31kadhalika na hao wameasi sasa, ili kwa kupata rehema kwenu wao nao wapate rehema. 32#Gal 3:22; 1 Tim 2:4 Maana Mungu amewafunga wote pamoja katika kuasi ili awarehemu wote.
33 # Isa 55:8; 45:15; Rum 9:23; 10:12 Jinsi zilivyo kuu utajiri na hekima na maarifa ya Mungu! Hukumu zake hazichunguziki, wala njia zake hazieleweki! 34#Isa 40:13; Ayu 15:8; Yer 23:18; 1 Kor 2:16 Maana ni nani aliyeijua nia ya Bwana? Au ni nani aliyekuwa mshauri wake? 35#Ayu 41:11 Au ni nani aliyempa yeye kitu kwanza, naye atalipwa tena? 36#1 Kor 8:6 Kwa kuwa vitu vyote vyatoka kwake, viko kwa uweza wake, tena vinarejea kwake. Utukufu una yeye milele. Amina.

Iliyochaguliwa sasa

Warumi 11: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha