Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ufunuo 16

16
Ghadhabu ya Mungu
1 # Isa 66:6; Zab 69:24; Yer 10:25; Sef 3:8 Nikasikia sauti kuu kutoka hekaluni, ikiwaambia wale malaika saba, Nendeni mkayamwage yale mabakuli saba ya ghadhabu ya Mungu juu ya nchi.
2 # Kut 9:10,11; Kum 28:35 Akaenda huyo wa kwanza, akalimimina bakuli lake juu ya nchi; pakawa na jipu baya, bovu, juu ya wale watu wenye chapa ya huyo mnyama, na wale wenye kuisujudia sanamu yake.
3 # Kut 7:17-21 Na huyo wa pili akalimimina bakuli lake juu ya bahari, ikawa damu, kama damu ya maiti, na vitu vyote vyenye roho ya uhai katika bahari vikafa.
4 # Kut 7:17-21; Zab 78:44 Na huyo wa tatu akalimimina bakuli lake juu ya mito na chemchemi za maji; zikawa damu. 5#Zab 119:137; 145:17; Kut 3:14; Kum 32:4; Isa 41:4 Nami nikamsikia malaika wa maji akisema, Wewe u mwenye haki, uliyeko na uliyekuwako, Mtakatifu, kwa kuwa umehukumu hivi; 6#Isa 49:26; Zab 79:3 kwa kuwa walimwaga damu ya watakatifu na ya manabii, nawe umewapa damu wainywe; ndiyo wanayostahili. 7#Zab 19:9; 119:137; Ufu 9:13; 19:2 Nikaisikia hiyo madhabahu ikisema, Naam, Bwana Mungu Mwenyezi, hukumu zako ni za kweli, na haki.
8Na huyo wa nne akalimimina bakuli lake juu ya jua, nalo likaruhusiwa kuwaunguza wanadamu kwa moto. 9#Ufu 9:20,21; 11:18 Wanadamu wakaunguzwa na joto kali, nao wakalitukana jina la Mungu aliye na mamlaka juu ya mapigo hayo; wala hawakutubu wala kumpa utukufu.
10 # Kut 10:21; Isa 8:21,22 Na huyo wa tano akalimimina bakuli lake juu ya kiti cha enzi cha yule mnyama; ufalme wake ukatiwa giza; wakatafuna ndimi zao kwa sababu ya maumivu, 11#Dan 2:19 wakamtukana Mungu wa mbingu kwa sababu ya maumivu yao, na kwa sababu ya majipu yao; wala hawakuyatubia matendo yao.
12 # Isa 11:15; 41:2; 44:27; Mwa 15:18; Kum 1:7; Yos 1:4; Yer 50:38 Na huyo wa sita akalimimina bakuli lake juu ya mto ule mkubwa Frati; maji yake yakakauka, ili njia itengenezwe kwa wafalme watokao katika maawio ya jua. 13#Ufu 12:9; 13:1,11; Kut 8:3; 1 Fal 22:21-23 Nikaona roho tatu za uchafu zilizofanana na vyura, zikitoka katika kinywa cha lile joka, na katika kinywa cha yule mnyama, na katika kinywa cha yule nabii wa uongo. 14#Ufu 13:13; 19:19 Hizo ndizo roho za mashetani, zifanyazo ishara, zitokazo na kuwaendea wafalme wa ulimwengu wote kuwakusanya kwa vita ya siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi. 15#Mt 24:43-44; Lk 12:39-40; Ufu 3:3,18; 1 The 5:2 (Tazama, naja kama mwizi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake.) 16#2 Fal 9:27; 23:29; Zek 12:11; Amu 5:19,31 Wakawakusanya hadi mahali paitwapo kwa Kiebrania, Harmagedoni.
17 # Isa 66:6 Na huyo wa saba akalimimina bakuli lake juu ya anga. Sauti kuu ikatoka katika hekalu, katika kile kiti cha enzi, ikisema, Imekwisha kuwa. 18#Ufu 4:5; 8:5; 11:13,19; Kut 19:16; Dan 12:1 Pakawa na umeme na sauti na radi; na palikuwa na tetemeko la nchi kubwa, ambalo tangu wanadamu kuwako juu ya nchi hapajawa namna ile, jinsi lilivyokuwa kubwa tetemeko hilo. 19#Isa 51:17; Dan 4:30; Yer 25:15; Ufu 14:10 Na mji ule mkuu ukagawanyika katika mafungu matatu, na miji ya mataifa ikaanguka; na Babeli ule mkuu ukakumbukwa mbele za Mungu, kupewa kikombe cha mvinyo ya ghadhabu ya hasira yake. 20#Ufu 6:14; 20:11 Kila kisiwa kikakimbia, wala milima haikuonekana tena. 21#Kut 9:23; Ufu 11:19 Na mvua ya mawe kubwa sana, ya mawe mazito kama talanta, ikashuka kutoka mbinguni juu ya wanadamu. Wanadamu wakamtukana Mungu kwa sababu ya lile pigo la mvua ya mawe; kwa maana pigo lake ni kubwa mno.

Iliyochaguliwa sasa

Ufunuo 16: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha