Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 84

84
Shangwe ya kuabudu katika hekalu
Kwa mwimbishaji: kwa mtindo wa Gitithi. Ya Wakorahi. Zaburi.
1 # Zab 26:8; 27:4; Ebr 9:23,24; Ufu 21:2,3 Maskani zako zapendeza kama nini,
Ee BWANA wa majeshi!
2Nafsi yangu imezionea shauku nyua za BWANA,
Naam, na kuzikondea.
Moyo wangu na mwili wangu
Vinamlilia Mungu aliye hai.
3Hata Shomoro ameona nyumba,
Na mbayuwayu amejipatia kiota,
Alipoweka makinda yake,
Kwenye madhabahu zako, Ee BWANA wa majeshi,
Mfalme wangu na Mungu wangu.
4Heri wakaao nyumbani mwako,
Wanakuhimidi daima.
5Heri ambaye nguvu zake zatoka kwako,
Na njia ziendazo Sayuni zimo moyoni mwake.
6Wapitapo katika bonde la baraka,
Hulifanya kuwa chemchemi,
Naam, mvua ya vuli hulijaza baraka.
7 # Kum 16:16 Huendelea toka nguvu hata nguvu,
Huonekana Sayuni kila mmoja mbele za Mungu.
8BWANA, Mungu wa majeshi, uyasikie maombi yangu,
Ee Mungu wa Yakobo, usikilize, wako.
9 # Mwa 15:1 Ee Mungu, ngao yetu, uangalie,
Umtazame uso masihi#84:9 Au, mtiwa mafuta.
10Hakika siku moja katika nyua zako
Ni bora kuliko siku elfu kwingineko;
Ningependa kuwa bawabu nyumbani mwa Mungu wangu,
Kuliko kuishi katika hema za uovu.
11Kwa kuwa BWANA, Mungu, ni jua na ngao,
BWANA atatoa neema na utukufu.
Hatawanyima kitu chema
Hao waendao kwa ukamilifu.
12Ee BWANA wa majeshi,
Heri mwanadamu anayekutumaini Wewe.

Iliyochaguliwa sasa

Zaburi 84: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha