Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 65

65
Shukrani kwa mavuno mengi
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. Wimbo.
1Ee Mungu, wastahili sifa katika Sayuni,
Na kwako Wewe itaondolewa nadhiri.
2 # Lk 11:9,10; Isa 66:23 Wewe usikiaye maombi,
Wote wenye mwili watakujia.
3 # Ebr 9:14 Tutakapozidiwa na matendo maovu
Wewe utatuondolea uovu wetu.
4 # Zab 33:12 Heri mtu yule umchaguaye,
Na kumkaribisha akae nyuani mwako.
Na tushibe wema wa nyumba yako,
Patakatifu pa hekalu lako.
5Kwa mambo ya kutisha utatujibu,
Katika haki, Ee Mungu wa wokovu wetu.
Wewe uliye tumaini la miisho yote ya dunia,
Na la bahari iliyo mbali sana,
6Milima waiweka imara kwa nguvu zako,
Huku ukijifunga uweza kama mshipi.
7 # Mt 8:26 Watuliza kuvuma kwa bahari,
Kuvuma kwa mawimbi yake,
Na ghasia za watu;
8 # Ayu 37:5 Kwa hiyo wakaao mbali kabisa huogopa ishara zako;
Milango ya asubuhi na jioni waifurahisha.
9Umeijia nchi na kuisitawisha,
Umeitajirisha sana;
Mto wa Mungu umejaa maji;
Wawapa watu nafaka
Maana ndiwe uitengenezaye ardhi.
10Matuta yake wayajaza maji;
Wapasawazisha palipoinuka,
Wailainisha nchi kwa manyunyu;
Waibariki mimea yake.
11 # Zab 104:3 Umeuvika mwaka taji la wema wako;
Mapito yako yadondoza unono.
12Huyadondokea malisho ya nyikani,
Na vilima vimejawa na furaha.
13Na malisho yamejawa na kondoo,
Na mabonde yamepambwa nafaka,
Yanashangilia, na kuimba pamoja kwa shangwe.

Iliyochaguliwa sasa

Zaburi 65: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha