Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 37:21-40

Zaburi 37:21-40 SRUV

Asiye haki hukopa wala halipi, Bali mwenye haki hufadhili, hukirimu. Maana waliobarikiwa na BWANA watairithi nchi, Nao waliolaaniwa naye watakatiliwa mbali. Hatua za mtu mwema huimarishwa na BWANA, Naye huipenda njia yake. Ajapojikwaa hataanguka chini, Maana BWANA humshika mkono na kumtegemeza. Nilikuwa kijana na sasa ni mzee, Lakini sijamwona mwenye haki ameachwa Wala mzawa wake akiomba chakula. Mchana kutwa hufadhili na kukopesha, Na mzao wake hubarikiwa. Jiepushe na uovu, utende mema, Na kukaa hata milele. Kwa kuwa BWANA hupenda haki, Wala hawaachi watauwa wake. Wao hulindwa milele, Bali mzawa wa wasio haki ataharibiwa. Wenye haki watairithi nchi, Nao watakaa humo milele. Kinywa chake mwenye haki hunena hekima, Na ulimi wake husema hukumu. Sheria ya Mungu wake imo moyoni mwake. Hatua zake hazitelezi. Mtu asiye haki humvizia mwenye haki, Na kutafuta jinsi ya kumwua. BWANA hatamwacha mkononi mwake, Wala hatamwacha alaumiwe atakapohukumiwa. Wewe umngoje BWANA, Uishike njia yake, Naye atakutukuza uirithi nchi, Utawaona Wasio haki wakiangamizwa. Nimemwona mtu asiye haki mkali sana, Akijieneza kama mwerezi wa Lebanoni. Nikapita na kumbe! Hayuko, Nikamtafuta wala hakuonekana. Umwangalie sana mtu mkamilifu, Umtazame mtu mnyofu, Maana mwisho wake mtu huyo ni amani. Wakosaji wataangamizwa pamoja, Wasio haki mwisho wao wataharibiwa. Na wokovu wa wenye haki una BWANA; Yeye ni ngome yao wakati wa taabu. Naye BWANA huwasaidia na kuwaopoa; Huwaopoa kutoka kwa wasio haki na kuwaponya; Kwa kuwa wamemtumaini Yeye.

Soma Zaburi 37

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Zaburi 37:21-40

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha