Mbingu zauhubiri utukufu wa Mungu, Na anga laitangaza kazi ya mikono yake. Mchana husemezana na mchana, Usiku hutolea usiku maarifa. Hakuna usemi wala maneno, Sauti yao haisikilikani. Sauti yao imeenea duniani kote, Na maneno yao hadi miisho ya ulimwengu. Katika hizo ameliwekea jua hema, Nalo hutokeza kama bwana arusi akitoka chumbani mwake, Lafurahi kama mtu aliye hodari Kwenda mbio katika njia yake. Kuchomoza kwake ni katika mwisho wa mbingu, Na kuzunguka kwake ni hadi miisho ya mbingu, Wala hakuna kitu Kisichofikiwa na joto lake.
Soma Zaburi 19
Shirikisha
linganisha matoleo yote: Zaburi 19:1-6
Hifadhi mistari, soma bila mtandao, tazama klipu za mafunzo, na zaidi!
YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha
Nyumbani
Biblia
Mipango
Video