Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 107:23-43

Zaburi 107:23-43 SRUV

Washukao baharini katika merikebu, Wafanyao kazi yao katika maji mengi, Hao huziona kazi za BWANA, Na maajabu yake vilindini. Maana alisema, akavumisha upepo wa dhoruba, Ukayainua juu mawimbi ya bahari. Walirushwa juu mbinguni, waliteremka hadi vilindini, Uhodari wao ukayeyuka katika maafa yao. Waliyumbayumba, walipepesuka kama mlevi, Ujuzi wao wote uliwaishia. Wakamlilia BWANA katika dhiki zao, Akawaponya kutoka kwa shida zao. Huituliza dhoruba, ikawa shwari, Mawimbi yake yakanyamaza. Ndipo walipofurahi kwa kuwa yametulia Naye akawaleta mpaka bandani waliyoitamani. Na wamshukuru BWANA kwa fadhili zake, Na maajabu yake kwa wanadamu. Na wamtukuze katika kusanyiko la watu, Na wamhimidi katika baraza la wazee. Amegeuza mito ikawa jangwa, Na chemchemi za maji zikawa nchi kavu. Nchi ya matunda mengi ikawa uwanda wa chumvi, Kwa sababu ya uovu wa wakazi wake. Amegeuza jangwa ikawa ziwa la maji, Na nchi kavu ikawa chemchemi za maji. Maana amewakalisha huko wenye njaa, Nao wamejenga mji wa kukaa. Wakapanda mbegu katika mashamba, Na kutia mizabibu iliyotoa matunda yake. Naye aliwabariki wakaongezeka sana, Wala hawapunguzi mifugo wao. Walipopungua na kudhilika, Kwa kuonewa na dhiki na huzuni. Aliwamwagia wakuu dharau, Na kuwazungusha katika nyika isiyo na njia. Lakini alimwinua mhitaji juu mbali na mateso, Na kuwaongeza jamaa zao kama kundi la kondoo. Wanyofu wa moyo wanaona na kufurahi, Na waovu wote wananyamazishwa. Aliye na hekima na ayaangalie hayo; Na wazitafakari fadhili za BWANA.

Soma Zaburi 107