Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Nehemia 6:15-19

Nehemia 6:15-19 SRUV

Basi huo ukuta ukakamilika siku ya ishirini na tano ya mwezi wa Eluli, katika muda wa siku hamsini na mbili. Ikawa adui zetu wote waliposikia, ndipo wamataifa wote waliotuzunguka wakaogopa, nao wakakata tamaa sana machoni pao wenyewe; maana waliitambua kazi hiyo ilivyotendwa na Mungu wetu. Tena siku zile wakuu wa Yuda walimtumia nyaraka nyingi Tobia nazo nyaraka za Tobia ziliwafikia. Kwa maana walikuwa watu wengi katika Yuda waliomwapia, kwa sababu alikuwa mkwewe Shekania, mwana wa Ara; naye Yehohanani mwanawe amemwoa binti Meshulamu, mwana wa Berekia. Tena waliyanena mema yake mbele yangu, na kumwambia maneno yangu. Tobia naye akaniletea mimi nyaraka za kuniogofya.

Soma Nehemia 6