Marko 7:31-35
Marko 7:31-35 SRUV
Akatoka tena katika mipaka ya Tiro, akapita katikati ya Sidoni, akaenda mpaka ziwa la Galilaya, kati ya mipaka ya Dekapoli. Wakamletea kiziwi, naye ni mwenye utasi, wakamsihi amwekee mikono. Akamtenga na mkutano faraghani, akatia vidole vyake masikioni mwake, akatema mate, akamgusa ulimi, akatazama juu mbinguni, akapiga kite, akamwambia, Efatha, maana yake, Funguka. Mara masikio yake yakafunguka, kifungo cha ulimi wake kikalegea, akasema vizuri.




