Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Marko 10

10
Mafundisho juu ya talaka
1 # Mt 19:1-9 Akaondoka huko akafika katika eneo la Yudea, na ng'ambo ya Yordani; makutano mengi wakakutanika tena wakamwendea; akawafundisha tena kama alivyozoea.#Mk 9:33 2Basi Mafarisayo wakamwendea, wakamwuliza, Je! Ni halali mtu kumwacha mkewe? Huku wakimjaribu. 3Naye akajibu, akawaambia, Musa aliwaamuru nini? 4#Kum 24:1-4; Mt 5:31,32 Wakasema, Musa alitoa ruhusa kuandika hati ya talaka na kumwacha. 5Yesu akawaambia, Kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu aliwaandikia amri hii. 6#Mwa 1:27; 5:2 Lakini tangu mwanzo wa kuumbwa ulimwengu, aliwaumba mwanamume na mwanamke. 7#Mwa 2:24 Kwa sababu hiyo mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; 8na hao wawili watakuwa mwili mmoja; hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. 9Basi alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe. 10Ndipo nyumbani tena wanafunzi wakamwuliza habari ya neno hilo. 11#Mt 5:32; 1 Kor 7:10-11 Akawaambia, Kila mtu atakayemwacha mkewe na kuoa mwingine azini juu yake;#Lk 16:18 12na mke, akimwacha mumewe na kuolewa na mtu mwingine, azini.
Yesu awabariki watoto wadogo
13 # Mt 19:13-15; Lk 18:15-17 Basi wakamletea watoto wadogo ili awaguse; wanafunzi wake wakawakemea. 14Ila Yesu alipoona alichukizwa sana, akawaambia, Waacheni watoto wadogo waje kwangu, msiwazuie; kwa maana watoto kama hawa ufalme wa Mungu ni wao. 15#Mt 18:3 Amin, nawaambieni, yeyote asiyeukubali ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo hatauingia kabisa. 16#Mk 9:36 Akawakumbatia, akaweka mikono yake juu yao, akawabariki.
Mtu aliyekuwa tajiri
17 # Mt 19:16-30; Lk 18:18-30 Alipokuwa akitoka kwenda njiani, mtu mmoja akaja mbio, akampigia magoti, akamwuliza, Mwalimu mwema, nifanye nini nipate kuurithi uzima wa milele? 18Yesu akamwambia, Kwa nini kuniita mwema? Hakuna aliye mwema ila mmoja, ndiye Mungu. 19#Kut 20:12-16; Kum 5:16-20; 24:14 Wazijua amri, Usiue, Usizini, Usiibe, Usishuhudie uongo, Usidanganye, Waheshimu baba yako na mama yako. 20Akamwambia, Mwalimu, haya yote nimeyashika tangu utoto wangu. 21#Mk 8:34; Mt 10:38 Yesu akamkazia macho, akampenda, akamwambia, Umepungukiwa na neno moja. Nenda, ukauze ulivyo navyo vyote, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha njoo unifuate. 22Lakini yeye akakunja uso kwa neno hilo, akaenda zake kwa huzuni; kwa sababu alikuwa na mali nyingi.
23Yesu akatazama kotekote, akawaambia wanafunzi wake, Jinsi itakavyokuwa shida wenye mali kuingia katika ufalme wa Mungu! 24#Zab 62:10; 1 Tim 6:17 Wanafunzi wakashangaa kwa maneno yake. Yesu akajibu tena, akawaambia, Watoto, jinsi ilivyo shida wenye kutegemea mali kuingia katika ufalme wa Mungu! 25Ni rahisi ngamia kupenya katika tundu ya sindano kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu. 26Nao wakashangaa mno, wakimwambia, Ni nani, basi, awezaye kuokoka? 27#Mwa 18:14; Ayu 42:2 Yesu akawakazia macho, akasema, Kwa wanadamu haiwezekani, bali kwa Mungu sivyo; maana yote yawezekana kwa Mungu. 28Petro akaanza kumwambia, Tazama, sisi tumeacha vyote tukakufuata wewe. 29Yesu akasema, Amin, nawaambieni, Hakuna mtu aliyeacha nyumba, au ndugu wa kiume, au ndugu wa kike, au mama, au baba, au watoto, au mashamba, kwa ajili yangu, na kwa ajili ya Injili, 30ila atapewa mara mia sasa wakati huu, nyumba, na ndugu wa kiume, na ndugu wa kike, na mama, na watoto, na mashamba, pamoja na udhia; na katika ulimwengu ujao uzima wa milele. 31#Mt 20:16; Lk 13:30 Lakini wengi walio wa kwanza watakuwa wa mwisho; na wa mwisho watakuwa wa kwanza.
Yesu asema juu ya kufa na kufufuka kwake kwa mara ya tatu
32 # Mt 20:17-19; Lk 18:31-34 Nao walikuwako njiani, huku wakipanda kwenda Yerusalemu; na Yesu alikuwa akiwatangulia, wakashangaa, nao katika kufuata wakaogopa. Akawatwaa tena wale Kumi na Wawili, akaanza kuwaambia kuhusu mambo yatakayompata,#Yn 11:16,55; Mk 9:31 33akisema, Angalieni, tunapanda kwenda Yerusalemu; na Mwana wa Adamu atatiwa mikononi mwa wakuu wa makuhani na waandishi, nao watamhukumu afe, watamtia mikononi mwa Mataifa, 34nao watamdhihaki, na kumtemea mate, na kumpiga mijeledi, na kumwua; na baada ya siku tatu atafufuka.
Ombi la Yakobo na Yohana
35 # Mt 20:20-28 Na Yakobo na Yohana, wana wa Zebedayo, wakamwendea, wakamwambia, Mwalimu, twataka utufanyie lolote tutakalokuomba. 36Akawaambia, Mwataka niwafanyie nini? 37Wakamwambia, Utujalie sisi tuketi, mmoja mkono wako wa kulia, na mmoja mkono wako wa kushoto, katika utukufu wako. 38#Lk 12:50; Mk 14:36; Rum 6:3 Yesu akawaambia, Hamjui mnaloliomba. Mwaweza kunywea kikombe ninyweacho mimi, au kubatizwa ubatizo nibatizwao mimi? 39#Mdo 12:2; Ufu 1:9 Wakamwambia, Twaweza. Yesu akawaambia, Kikombe ninyweacho mimi mtakinywea, na ubatizo nibatizwao mimi mtabatizwa; 40lakini kuhusu kuketi katika mkono wangu wa kulia au mkono wangu wa kushoto si langu kuwapa, ila wao watapewa waliowekewa tayari. 41Hata wale kumi waliposikia wakaanza kuwakasirikia Yakobo na Yohana. 42#Lk 22:25-26 Yesu akawaita, akawaambia, Mwajua ya kuwa wale wanaohesabiwa kuwa wakuu wa Mataifa huwatawala kwa nguvu, na wakubwa wao huwatumikisha. 43#Mt 23:11; Mk 9:35; Lk 22:26 Lakini haitakuwa hivyo kwenu; bali mtu anayetaka kuwa mkubwa kwenu, atakuwa mtumishi wenu, 44na mtu anayetaka kuwa wa kwanza wenu, atakuwa mtumwa wa wote. 45Kwa maana Mwana wa Adamu naye hakuja kutumikiwa, bali kutumika, na kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi.
Kuponywa kwa kipofu Bartimayo
46 # Mt 20:29-34; Lk 18:35-43 Wakafika Yeriko; alipokuwa akiondoka kutoka Yeriko, pamoja na wanafunzi wake, na mkutano mkubwa, mwana wa Timayo, Bartimayo, yule mwombaji kipofu, alikuwa ameketi kando ya njia. 47Naye aliposikia ya kwamba ni Yesu Mnazareti, alianza kupaza sauti yake, na kusema, Mwana wa Daudi, Yesu, unirehemu. 48Na wengi wakamkemea ili anyamaze, lakini alizidi kupaza sauti, Mwana wa Daudi, unirehemu. 49Yesu akasimama akasema, Mwiteni. Wakamwita yule kipofu, wakamwambia, Jipe moyo; inuka, anakuita. 50Akatupa vazi lake, akaruka, akamwendea Yesu. 51Yesu akamjibu, akamwambia, Wataka nikufanyie nini? Yule kipofu akamwambia, Mwalimu wangu, nataka nipate kuona. 52Yesu akamwambia, Nenda zako, imani yako imekuponya. Mara akapata kuona; akamfuata njiani.

Iliyochaguliwa sasa

Marko 10: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha