Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mathayo 17

17
Kugeuka sura
1 # 2 Pet 1:17-18 Na baada ya siku sita Yesu akawatwaa Petro, na Yakobo, na Yohana nduguye, akawaleta juu ya mlima mrefu faraghani; 2#2 Pet 1:16-18 akageuka sura yake mbele yao; uso wake ukang'aa kama jua, mavazi yake yakawa meupe kama nuru. 3Na tazama, wakatokewa na Musa na Eliya, wakizungumza naye. 4Petro akajibu akamwambia Yesu, Bwana, ni vizuri sisi kuwapo hapa; ukitaka, nitafanya hapa vibanda vitatu, kimoja chako wewe, na kimoja cha Musa, na kimoja cha Eliya. 5#Mwa 22:2; Kum 18:15; Zab 2:7; Isa 42:1; Mt 3:17; 12:18; Mk 1:11; Lk 3:22 Alipokuwa bado akisema, tazama, wingu jeupe likawatia uvuli; na tazama, sauti ikatoka katika lile wingu, ikasema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye; msikieni yeye. 6Na wale wanafunzi waliposikia, walianguka kifudifudi na kuogopa sana. 7Yesu akaja, akawagusa, akasema, Inukeni, wala msiogope. 8Wakainua macho yao, wasione mtu ila Yesu peke yake.
9 # Mt 16:20 Na walipokuwa wakishuka mlimani, Yesu aliwaagiza, akasema, Msimwambie mtu yeyote habari ya maono hayo, hadi Mwana wa Adamu atakapofufuka katika wafu. 10#Mal 4:5; Mt 11:14 Wanafunzi wake wakamwuliza, wakisema, Basi kwa nini waandishi hunena ya kwamba imempasa Eliya kuja kwanza? 11Naye akajibu, akawaambia, Kweli Eliya yuaja kwanza, naye atatengeneza yote, 12#Mt 11:14; 14:9,10 ila nawaambia, ya kwamba Eliya amekwisha kuja, wasimtambue, lakini wakamtenda yote waliyotaka. Vivyo hivyo Mwana wa Adamu naye yuaenda kuteswa kwao. 13#Lk 1:17 Ndipo wale wanafunzi walipofahamu ya kuwa amesema nao habari za Yohana Mbatizaji.
Yesu aponya mvulana mwenye pepo
14 # Mk 9:14-29; Lk 9:37-42 Nao walipoufikia mkutano, mtu mmoja akamjia, akampigia magoti, akisema, 15Bwana, umrehemu mwanangu, kwa kuwa ana kifafa, na kuteswa vibaya; maana mara nyingi huanguka motoni, na mara nyingi majini. 16Nilimleta kwa wanafunzi wako, wasiweze kumponya. 17#Kum 32:5; Yn 14:9 Yesu akajibu, akasema, Enyi kizazi kisichoamini, kilichopotoka, nitakaa pamoja nanyi hadi lini? Nitachukuliana nanyi hadi lini? Mleteni huku kwangu. 18Yesu akamkemea pepo, naye akamtoka; yule mvulana akapona tangu saa ile. 19#Mt 10:1 Kisha wale wanafunzi wakamwendea Yesu kwa faragha wakasema Mbona sisi hatukuweza kumtoa? 20#Mt 21:21; Mk 11:23; 1 Kor 13:2; Lk 17:6 Yesu akawaambia, Kwa sababu ya upungufu wa imani yenu. Kwa maana, amin, nawaambia, Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu. [ 21Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga.]
Yesu asema tena juu ya kufa na kufufuka kwake
22 # Mk 9:30-32; Lk 9:43-45 Nao walipokuwa wakikaa Galilaya, Yesu akawaambia, Mwana wa Adamu anakwenda kutiwa katika mikono ya watu, nao watamwua, na siku ya tatu atafufuka.#Mt 16:21 23Wakasikitika sana.
Yesu na ushuru wa hekalu
24 # Kut 30:13; 38:26 Na walipofika Kapernaumu, wale watozao nusu-shekeli walimwendea Petro, wakasema, Je! Mwalimu wenu hatoi ushuru wa hekalu?#17:24 yaani nusu shekeli. Akasema, Hutoa. 25Naye alipoingia nyumbani, Yesu alitangulia kumwuliza, akisema, Waonaje, Simoni? Wafalme wa dunia hutwaa kodi ama ushuru kwa watu gani? Kwa wana wao au kwa wageni? 26Naye aliposema, Kwa wageni, Yesu alimwambia, Basi, kama ni hivyo, wana wako huru. 27Lakini tusije tukawakwaza, nenda baharini ukatupe ndoana, ukatwae samaki yule azukaye kwanza; na ukifumbua mdomo wake utaona shekeli;#17:27 Shekeli moja ni kama shilingi 3. ichukue hiyo ukawape kwa ajili yangu na kwa ajili yako.

Iliyochaguliwa sasa

Mathayo 17: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha