Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mambo ya Walawi 17

17
Uchinjaji wa wanyama
1BWANA akamwambia Musa 2Sema na Haruni, na wanawe, na wana wote wa Israeli, uwaambie; Neno hili ndilo aliloamuru BWANA, 3Mtu yeyote wa nyumba ya Israeli atakayechinja ng'ombe, mwana-kondoo, au mbuzi, ndani au nje ya kambi, 4#Kum 12:5; Zab 32:2; Rum 4:6; 5:13; Mwa 17:14 wala hamleti mlangoni pa hema ya kukutania, kama matoleo kwa BWANA mbele ya hema ya BWANA; mtu huyo atahesabiwa kuwa ana hatia ya damu; amemwaga damu; na atatupiliwa mbali na watu wake; 5#Mwa 21:33; 22:2; Kum 12:2; 1 Fal 14:22,23; 2 Fal 17:10; Eze 20:28; 22:9 ili wana wa Israeli walete sadaka zao, wazichinjazo mashambani, wazilete kwa BWANA, mpaka mlango wa hema ya kukutania, kwa huyo kuhani, ili wazichinje ziwe sadaka za amani kwa BWANA. 6#Kut 29:18; Law 4:31; Hes 18:17 Naye kuhani atainyunyiza damu yake juu ya madhabahu ya BWANA, mlangoni pa hema ya kukutania, na kuyateketeza mafuta yake, yawe harufu njema mbele za BWANA. 7#Kum 32:17; 2 Nya 11:15; Zab 106:37; Mdo 7:42,43; 1 Kor 10:20; Kut 34:15; Kum 31:16 Wala hawatatoa tena sadaka zao kwa wale majini, ambao huwafuata ili wafanye uasherati nao. Sheria hii itakuwa sheria ya milele kwao, kizazi baada ya kizazi.
8Nawe utawaambia, Mtu yeyote katika nyumba ya Israeli, au miongoni mwa wageni, wanaokaa nao, atoaye sadaka ya kuteketezwa au dhabihu, 9wala haileti mlangoni pa hema ya kukutania, ili aisongeze kwa BWANA basi mtu huyo atatengwa na watu wake.
Katazo la kula damu
10 # Mwa 9:4; Law 7:26-27; 19:26; Kum 12:16,23; 15:23; 1 Sam 14:33; Law 26:17; Yer 44:11; Eze 15:7 Kisha mtu yeyote wa nyumba ya Israeli, au miongoni mwa hao wageni wakaao kati yao, atakayekula damu, ya aina yoyote, nitamkataa mtu huyo alaye damu, na nitamtenga na watu wake. 11#Ebr 9:22; Mk 14:24; Rum 5:9; Efe 1:7; Kol 1:14; 1 Pet 1:2; 1 Yoh 1:7 Kwa kuwa uhai wa mwili uko katika hiyo damu; nami nimewapa ninyi hiyo damu juu ya madhabahu, ili kufanya upatanisho kwa ajili ya nafsi zenu; kwani ni hiyo damu ifanyayo upatanisho kwa sababu ya nafsi. 12Kwa hiyo niliwaambia wana wa Israeli, Hapana mtu miongoni mwenu aliye na ruhusa kula damu, wala mgeni aishiye kati yenu asile damu.
13 # Kum 12:16; 15:23; 1 Sam 14:32-34; Eze 24:7 Mtu yeyote aliye wa wana wa Israeli, au wa hao wageni wakaao kati yenu, ambaye amemshika mnyama, au ndege ambaye huliwa, katika kuwinda kwake; atamwaga damu yake, na kuifunikia mchangani. 14#Mwa 9:4 Kwa kuwa uhai wa kila kiumbe uko katika damu yake; ndio nikawaagiza wana wa Israeli, Msiile damu ya mnyama wa aina yoyote; kwa kuwa uhai wa kila kiumbe ni damu yake; yeyote atakayeila atatengwa. 15#Kut 22:31; Kum 14:21; Eze 4:14 Tena kila mtu atakayekula nyamafu, au nyama ya mnyama aliyeraruliwa na wanyama, awe ni mzalia au mgeni, atafua nguo zake, na kuoga majini naye atakuwa najisi hadi jioni; ndipo atakapokuwa safi. 16#Hes 19:20; Ebr 9:28 Lakini iwapo hazifui, wala haogi mwili, ndipo atakapolipizwa uovu wake.

Iliyochaguliwa sasa

Mambo ya Walawi 17: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha