Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maombolezo 2:1-6

Maombolezo 2:1-6 SRUV

Jinsi Bwana alivyomfunika binti Sayuni Kwa wingu katika hasira yake! Ameutupa toka mbinguni hata nchi Huo uzuri wa Israeli; Wala hakukikumbuka kiti cha miguu yake Katika siku ya hasira yake. Bwana ameyameza makao yote ya Yakobo, Wala hakuona huruma; Ameziangusha ngome za binti Yuda Katika ghadhabu yake; Amezibomoa hata nchi Ameunajisi ufalme na wakuu wake. Ameikata pembe yote ya Israeli Katika hasira yake kali; Ameurudisha nyuma mkono wake wa kulia Mbele ya hao adui, Naye amemteketeza Yakobo kama moto uwakao, Ulao pande zote. Ameupinda upinde wake kama adui, Amesimama na mkono wake wa kulia kama mtesi; Naye amewaua hao wote Waliopendeza macho; Katika hema ya binti Sayuni Amemimina ghadhabu yake kama moto. Bwana amekuwa mfano wa adui, Amemmeza Israeli; Ameyameza majumba yake yote, Ameziharibu ngome zake; Tena amemzidishia binti Yuda Matanga na maombolezo. Naye ameondoa maskani yake kwa nguvu, Kana kwamba ni ya bustani tu; Ameziharibu sikukuu zake; BWANA amezisahaulisha katika Sayuni Sikukuu na sabato; Naye amewadharau mfalme na kuhani Katika uchungu wa hasira yake.