Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ayubu 36:1-15

Ayubu 36:1-15 SRUV

Tena Elihu akaendelea na kusema, Ningojee kidogo nami nitakueleza; Kwa kuwa ningali na maneno kwa ajili ya Mungu. Nitayaleta maarifa yangu kutoka mbali, Nami nitampa haki Muumba wangu. Maana hakika maneno yangu si ya uongo; Aliyekamilika katika maarifa yu pamoja nawe. Tazama, Mungu ni hodari, wala hamdharau mtu yeyote; Ana uweza katika nguvu za fahamu. Hauhifadhi uhai wa waovu; Lakini huwapa wateswao haki yao. Yeye hawaondolei macho yake wenye haki; Lakini pamoja na wafalme huwaweka Katika viti vya enzi milele, nao hutukuzwa. Nao wakifungwa kwa pingu, Wakitwaliwa kwa kamba za mateso; Ndipo huwaonesha matendo yao, Na makosa yao, ya kuwa wametenda kwa kujivuna. Yeye huyafunua masikio yao, wasikie maonyo, Na kuwaagiza warudi kuuacha uovu. Kama wakisikia na kumtumikia, Watapisha siku zao katika kufanikiwa, Na miaka yao katika furaha. Lakini wasiposikia, wataangamia kwa upanga, Nao watakufa pasipo maarifa. Lakini hao wasiomcha Mungu mioyoni hujiwekea hasira Hawalilii msaada hapo awafungapo. Wao hufa wakingali vijana, Na uhai wao huangamia katikati ya wachafu. Yeye humponya aliyetaabika kwa njia ya taabu yake, Na kuyafunua masikio yao kwa maonevu.

Soma Ayubu 36