Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Waraka kwa Waebrania 13

13
Huduma impendezayo Mungu
1 # Yn 13:34; 2 Pet 1:7 Upendano wa ndugu na udumu. 2#Mwa 18:1-8; 19:1-3; Rum 12:13; 1 Pet 4:9 Msisahau kuwafadhili wageni; maana kwa njia hii wengine wamewakaribisha malaika pasipo kujua. 3#Mt 25:36 Wakumbukeni hao waliofungwa kana kwamba mmefungwa pamoja nao; na hao wanaodhulumiwa, kwa vile ninyi nanyi mlivyo katika mwili. 4#Gal 5:19,21; Efe 5:5 Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu. 5#Kum 31:6,8; Yos 1:5; 1 Tim 6:6 Msiwe na tabia ya kupenda fedha; muwe radhi na vitu mlivyo navyo; kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, Sitakupungukia kamwe, wala sitakuacha. 6#Zab 118:6 Hata tunathubutu kusema,
Bwana ndiye anisaidiaye, sitaogopa;
Mwanadamu atanitenda nini?
7 # 1 Kor 4:16 Wakumbukeni wale waliokuwa wakiwaongoza, waliowaambia neno la Mungu; tena, kwa kuuchunguza sana mwisho wa mwenendo wao, iigeni imani yao. 8#1 Kor 3:11; Ufu 1:17 Yesu Kristo ni yeye yule, jana na leo na hata milele. 9#Efe 4:14; Rum 14:17; 2 Kor 1:21 Msichukuliwe na mafundisho ya namna nyingine nyingine, na ya kigeni; maana ni vizuri moyo ufanywe imara kwa neema, wala si kwa vyakula, ambavyo wao waliokwenda navyo hawakupata faida. 10#Ebr 8:4,5 Tuna madhabahu ambayo wale waihudumiayo ile hema hawana ruhusa kula vitu vyake. 11#Law 16:27 Maana wanyama wale ambao damu yao huletwa ndani ya patakatifu na kuhani mkuu kwa ajili ya dhambi, viwiliwili vyao huteketezwa nje ya kambi. 12#Mt 21:39; Yn 9:22 Kwa ajili hii Yesu naye, ili awatakase watu kwa damu yake mwenyewe, aliteswa nje ya lango. 13#Ebr 11:26; 12:2 Basi na tutoke tumwendee nje ya kambi, tukichukua shutuma yake. 14#Ebr 11:10; 12:22 Maana hapa hatuna mji udumuo, bali twautafuta ule ujao. 15#Law 7:12; 2 Nya 29:31; Zab 50:14,23; Isa 57:19; Hos 14:2 Basi, kwa njia yake yeye, na tumpe Mungu dhabihu ya sifa daima, yaani, tunda la midomo iliungamalo jina lake. 16#Flp 4:18 Lakini msisahau kutenda mema na kushirikiana; maana sadaka kama hizi ndizo zimpendezazo Mungu.
17 # 1 The 5:12; Eze 3:17 Watiini viongozi wenu, na kuwanyenyekea; maana wao wanakesha kwa ajili ya roho zenu, kama watu watakaotoa hesabu, ili kwamba wafanye hivyo kwa furaha wala si kwa huzuni; maana haitawafaa ninyi.
18 # 2 Kor 1:12; Mdo 24:16 Tuombeeni; maana tunaamini kwamba tuna dhamiri njema, tukitaka kuwa na mwenendo mwema katika mambo yote. 19Nami nawasihi zaidi sana kufanya hayo ili nirudishwe kwenu upesi.
Baraka
20 # Isa 63:11; 55:3; Zek 9:11; Yer 32:40; Eze 37:26; Yn 10:12; 1 Pet 2:25 Basi, Mungu wa amani aliyemleta tena kutoka kwa wafu Mchungaji Mkuu wa kondoo, kwa damu ya agano la milele, yeye Bwana wetu Yesu, 21awafanye ninyi kuwa wakamilifu katika kila tendo jema, mpate kuyafanya mapenzi yake, naye akifanya ndani yetu lipendezalo mbele zake, kwa Yesu Kristo; utukufu una yeye milele na milele. Amina.
Mahimizo ya mwisho na salamu
22 # Yak 1:21 Lakini nawasihi, ndugu, mchukuliane na neno hili lenye maonyo maana nimewaandikia kwa maneno machache. 23Jueni ya kuwa ndugu yetu Timotheo amekwisha kufunguliwa; ambaye, akija upesi, nitaonana nanyi pamoja naye.
24Wasalimuni viongozi wenu wote, na watakatifu wote; hao walio wa Italia wanawasalimu.
25Neema na iwe nanyi nyote.

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha