Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Waraka kwa Waebrania 11

11
Maana ya imani
1 # Ebr 3:14; 2 Kor 5:7 Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni kusadiki mambo yasiyoonekana. 2Maana kwa hiyo wazee wetu walishuhudiwa. 3#Mwa 1:1; Zab 33:6,9; Yn 1:3 Kwa imani twafahamu ya kuwa ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu, hata vitu vinavyoonekana havikufanywa kwa vitu vilivyo dhahiri.
Mfano wa Habili, Henoko na Nuhu
4 # Mwa 4:3-10; Mt 23:35 Kwa imani Habili alimtolea Mungu dhabihu iliyo bora kuliko Kaini; kwa hiyo alishuhudiwa kuwa ana haki; Mungu akazishuhudia sadaka zake, na kwa hiyo, ijapokuwa amekufa, angali akinena. 5#Mwa 5:21-24 Kwa imani Henoko alihamishwa, asije akaona mauti, wala hakuonekana, kwa sababu Mungu alimhamisha; maana kabla ya kuhamishwa alikuwa ameshuhudiwa kwamba amempendeza Mungu. 6#Ebr 7:25; 10:35 Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao. 7#Mwa 6:8,9,13-22; 7:1; Rum 3:22,24; 4:20 Kwa imani Nuhu akiisha kuonywa na Mungu katika habari za mambo yasiyoonekana bado, kwa jinsi alivyomcha Mungu, aliunda safina, apate kuiokoa nyumba yake. Na hivyo akauhukumu makosa ulimwengu, akawa mrithi wa haki ipatikanayo kwa imani.
Imani ya Abrahamu
8 # Mwa 12:1-5 Kwa imani Abrahamu alipoitwa aliitika, atoke aende mahali pale atakapopapata kuwa urithi; akatoka asijue aendako. 9#Mwa 23:4; 26:3; 35:12,27 Kwa imani alikaa ugenini katika ile nchi ya ahadi, kama katika nchi isiyo yake, akikaa katika hema pamoja na Isaka na Yakobo, warithi pamoja naye wa ahadi ile ile. 10Maana alikuwa akiutazamia mji wenye misingi, ambao mwenye kuubuni na kuujenga ni Mungu. 11#Mwa 17:19; 18:11-14; 21:2 Kwa imani hata Sara mwenyewe alipokea uwezo wa kuwa na mimba; alipokuwa amepita wakati wake; kwa kuwa alimhesabu yeye aliyeahidi kuwa mwaminifu. 12#Mwa 15:5; 22:17; 32:12; Rum 4:19 Na kwa ajili ya hayo wakazaliwa na mtu mmoja, naye alikuwa kama mfu, watu wengi kama nyota za mbinguni wingi wao, na kama mchanga ulio ufuoni, usioweza kuhesabika.
13 # Mwa 23:4; 47:9; 1 Pet 1:1; 2:11; 1 Nya 29:15; Zab 39:12 Hawa wote wakafa katika imani, walikuwa hawajazipokea zile ahadi, bali wakaziona tokea mbali na kuzishangilia, na kukiri kwamba walikuwa wageni, na wasafiri juu ya nchi. 14Maana hao wasemao maneno kama hayo waonesha wazi kwamba wanatafuta nchi yao wenyewe. 15Na kama wangaliikumbuka nchi ile waliyotoka, wangalipata nafasi ya kurudi. 16#Kut 3:6; Mk 12:26,27 Lakini sasa wanaitamani nchi iliyo bora, yaani, ya mbinguni. Kwa hiyo Mungu haoni haya kuitwa Mungu wao; maana amewatengenezea mji.
17 # Mwa 22:1; Yak 2:22 Kwa imani Abrahamu alipojaribiwa, akamtoa Isaka awe dhabihu; na yeye aliyezipokea hizo ahadi alikuwa akimtoa mwanawe, mzaliwa pekee; 18#Mwa 21:12 naam, yeye aliyeambiwa, Katika Isaka uzao wako utaitwa, 19#Rum 4:17 akihesabu ya kuwa Mungu aweza kumfufua hata kutoka kuzimu; akampata tena toka huko kwa mfano. 20#Mwa 27:27-29,39-40 Kwa imani Isaka akawabariki Yakobo na Esau, hata kuhusu mambo yatakayokuwa baadaye. 21#Mwa 47:31—48:15,16,20 Kwa imani Yakobo, alipokuwa karibu kufa, akambariki kila mmoja wa wana wa Yusufu, akaabudu akiegemea kichwa cha fimbo yake. 22#Mwa 50:24-25; Kut 13:19 Kwa imani Yusufu, alipokuwa amekaribia mwisho wake, alitaja habari za kutoka kwao wana wa Israeli, akaagiza kuhusu mifupa yake.
Imani ya Musa
23 # Kut 2:2; 1:22 Kwa imani Musa, alipozaliwa, akafichwa miezi mitatu na wazazi wake, kwa sababu waliona kwamba ni mtoto mzuri; wala hawakuiogopa amri ya mfalme. 24#Kut 2:10-12 Kwa imani Musa alipokuwa mtu mzima, akakataa kuitwa mwana wa binti Farao; 25akaona ni afadhali kupata mateso pamoja na watu wa Mungu kuliko kujifurahisha katika dhambi kwa muda; 26#Zab 89:50; 69:9; Ebr 13:13; 10:34,35 akihesabu ya kuwa kushutumiwa kwake Kristo ni utajiri mkuu kuliko hazina za Misri; kwa kuwa aliyatazamia hayo malipo. 27#Kut 2:15; 12:51 Kwa imani akatoka Misri, asiogope ghadhabu ya mfalme; maana alistahimili kama amwonaye yeye asiyeonekana. 28#Kut 12:12,13,21-30 Kwa imani akaifanya Pasaka, na kule kunyunyiza damu, ili yule mwenye kuwaangamiza wazaliwa wa kwanza asiwaguse wao.
Imani ya mashujaa wengine Waisraeli
29 # Kut 14:21-31 Kwa imani wakapita kati ya Bahari ya Shamu, kama katika nchi kavu; Wamisri walipojaribu kufanya vivyo wakatoswa. 30#Yos 6:12-21 Kwa imani kuta za Yeriko zikaanguka, zilipokwisha kuzungukwa siku saba. 31#Yos 2:1-21; 6:17,22-25; Yak 2:25 Kwa imani Rahabu, yule kahaba, hakuangamia pamoja na hao walioasi; kwa kuwa aliwakaribisha wale wapelelezi kwa amani. 32#Amu 6:11—8:32; 4:6—5:31; 13:2—16:31; 11:1—12:7; 15:20; 1 Sam 16:1—1 Fal 2:11 Nami niseme nini tena? Maana wakati usingenitosha kuleta habari za Gideoni na Baraka na Samsoni na Yeftha na Daudi na Samweli na za manabii; 33#Dan 6:1-27; Amu 14:6; 1 Sam 17:34,35 ambao kwa imani walishinda milki za wafalme, walitenda haki, walipata ahadi, walifunga vinywa vya simba, 34#Dan 3:1-30 walizima nguvu za moto, waliokoka kutoka kwa makali ya upanga. Walitiwa nguvu baada ya kuwa dhaifu, walikuwa hodari katika vita, walikimbiza majeshi ya wageni. 35#1 Fal 17:17-24; 2 Fal 4:25-37 Wanawake walipokea wafu wao waliofufuliwa. Lakini wengine waliumizwa vibaya hata kuuawa, wasikubali ukombozi, ili wapate ufufuo ulio bora; 36#1 Fal 22:26-27; 2 Nya 18:25-26; Yer 20:2; 37:15; 38:6 wengine walijaribiwa kwa dhihaka na mapigo, naam, kwa minyororo, na kwa kutiwa gerezani; 37#2 Nya 24:21 walipigwa kwa mawe, walikatwa kwa misumeno, walijaribiwa, waliuawa kwa upanga; walizungukazunguka wakivaa ngozi za kondoo na ngozi za mbuzi; walikuwa wahitaji, wakiteswa, wakitendwa mabaya; 38(watu ambao ulimwengu haukustahili kuwa nao), walikuwa wakizungukazunguka katika nyika na katika milima na katika mapango na katika mashimo ya nchi. 39Na watu hao wote wakiisha kushuhudiwa kwa sababu ya imani yao, hawakuipokea ahadi; 40kwa kuwa Mungu alikuwa ametangulia kutuwekea sisi kitu kilicho bora, ili wao wasikamilishwe pasipo sisi.

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha