Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Waraka kwa Waebrania 1

1
Mungu amenena katika mwanaye
1Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi, 2#Zab 2:8; Yn 1:3; Kol 1:16; Mt 21:38 mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika Mwana, aliyemweka kuwa mrithi wa yote, tena kwa yeye aliufanya ulimwengu. 3#Zab 110:1; 2 Kor 4:4; Kol 1:15; Mk 16:19; Ebr 9:14,26 Yeye kwa kuwa ni mng'ao wa utukufu wa Mungu na chapa kamili ya nafsi yake, akivichukua vyote kwa amri ya uweza wake, akiisha kufanya utakaso wa dhambi, aliketi katika mkono wa kulia wa Ukuu huko juu; 4#Flp 2:9 amefanyika bora kupita malaika, kwa kadiri jina alilolirithi lilivyo tukufu kuliko lao.
Mwana ni mkuu kuliko Malaika
5 # Zab 2:7; 2 Sam 7:14; 1 Nya 17:14; Ebr 5:5; Mdo 13:33 Kwa maana ni kwa malaika yeyote yupi Mungu,
Ndiwe mwanangu,
Mimi leo nimekuzaa?
Na tena
Mimi nitakuwa kwake baba,
Na yeye atakuwa kwangu mwana?
6 # Kum 32:43; Rum 8:29; Zab 97:7 Hata tena, amletapo mzaliwa wa kwanza ulimwenguni, asema,
Na wamsujudu malaika wote wa Mungu.
7 # Zab 104:4 Na kuhusu malaika asema,
Awafanya malaika wake kuwa pepo,
Na watumishi wake kuwa miali ya moto.
8 # Zab 45:6-7 Lakini kuhusu Mwana asema,
Kiti chako cha enzi, Mungu, ni cha milele na milele;
Na fimbo ya ufalme wako ni fimbo ya haki.
9Umependa haki, umechukia maasi;
Kwa hiyo Mungu, Mungu wako, amekutia mafuta,
Mafuta ya shangwe kupita wenzio.
10 # Zab 102:25-27 Na tena,
Wewe, Bwana, hapo mwanzo uliitia misingi ya nchi,
Na mbingu ni kazi za mikono yako;
11Hizo zitaharibika, bali wewe unadumu;
Nazo zote zitachakaa kama nguo,
12Na kama mavazi utazikunjakunja, na kama mavazi zitabadilishwa;
Lakini wewe u yeye yule,
Na miaka yako haitakoma.
13 # Zab 110:1 Je! Yuko malaika aliyemwambia wakati wowote,
Uketi mkono wa kulia
Hata nitakapoweka adui zako chini ya nyayo zako?
14 # Dan 7:10; Zab 34:8; 91:11 Je! Hao wote si roho watumikao, wakitumwa kuwahudumia wale watakaourithi wokovu?

Iliyochaguliwa sasa

Waraka kwa Waebrania 1: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha