Kutoka 35:4-9
Kutoka 35:4-9 SRUV
Kisha Musa akanena na mkutano wote wa wana wa Israeli, akawaambia, Neno hili ndilo aliloliamuru BWANA, akisema, Katwaeni kati yenu matoleo kwa BWANA; mtu yeyote aliye na moyo wa kupenda, ayalete matoleo; dhahabu na fedha na shaba; na nyuzi za rangi ya buluu, zambarau, nyekundu, na kitani nzuri, na singa za mbuzi; na ngozi za kondoo dume zilizotiwa rangi nyekundu, ngozi za pomboo na mbao za mshita; na mafuta kwa hiyo taa, na viungo vya manukato kwa hayo mafuta ya kutiwa, na kwa huo uvumba mzuri; na vito vya shohamu, vito vya kutiwa kwa hiyo naivera na kwa hicho kifuko cha kifuani.