Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Amosi 9:13-15

Amosi 9:13-15 SRUV

Angalieni, siku zinakuja, asema BWANA, ambazo huyo alimaye atamfikia avunaye, na yeye akanyagaye zabibu atamfikia apandaye mbegu; nayo milima itadondoza divai tamu, na vilima vyote vitayeyuka. Nami nitawarejesha tena watu wangu Israeli waliohamishwa, nao wataijenga miji iliyoachwa maganjo, na kukaa ndani yake; nao watapanda mizabibu katika mashamba, na kunywa divai yake; nao watatengeneza bustani, na kula matunda yake. Nami nitawapanda katika nchi yao, wala hawatang'olewa tena watoke katika nchi yao niliyowapa, asema BWANA, Mungu wako.

Soma Amosi 9