Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 Wakorintho 4

4
Hazina katika vyombo vya udongo
1 # 2 Kor 3:6; 1 Kor 7:25 Kwa sababu hiyo, kwa kuwa tuna huduma hii, kwa jinsi tulivyopata rehema, hatulegei; 2#2 Kor 2:17; 1 The 2:5 lakini tumekataa mambo ya aibu yaliyositirika, wala hatuenendi kwa hila, wala kulichanganya neno la Mungu na uongo; bali kwa kuidhihirisha iliyo kweli twajionesha kuwa na haki, dhamiri za watu zikitushuhudia mbele za Mungu. 3#1 Kor 1:18 Lakini ikiwa Injili yetu imesitirika, imesitirika kwa hao wanaopotea; 4#Ebr 1:3; Efe 2:2; 2 The 2:11; Kol 1:15 ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, wasiione nuru ya Injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu. 5#2 Kor 1:24 Kwa maana hatujihubiri wenyewe, bali Kristo Yesu ya kuwa ni Bwana; na sisi wenyewe kuwa tu watumishi wenu kwa ajili ya Yesu. 6#Mwa 1:3; 2 Kor 3:18; Isa 9:1 Kwa kuwa Mungu, aliyesema, Nuru itang'aa toka gizani, ndiye aliyeng'aa mioyoni mwetu, atupe nuru ya elimu ya utukufu wa Mungu katika uso wa Yesu Kristo.
7 # 2 Kor 5:1; Mdo 9:15 Lakini tuna hazina hii katika vyombo vya udongo, ili adhama kuu ya uwezo iwe ya Mungu, wala si kutoka kwetu. 8#2 Kor 1:8; 7:5 Pande zote twateseka, bali hatusongwi; twaona shaka, bali hatukati tamaa; 9twaudhiwa, bali hatuachwi; twatupwa chini, bali hatuangamizwi; 10#1 Kor 15:31 siku zote twabeba katika mwili kuuawa kwake Yesu, ili uzima wa Yesu nao udhihirishwe katika miili yetu. 11#Rum 8:36 Kwa maana sisi tulio hai, siku zote twatolewa tufe kwa ajili ya Yesu, ili uzima wa Yesu nao udhihirishwe katika miili yetu ipatikanayo na mauti. 12Basi hapo mauti hufanya kazi ndani yetu, bali uzima ndani yenu. 13#Zab 116:10 Lakini kwa kuwa tuna roho ile ile ya imani; kama ilivyoandikwa, Niliamini, na kwa sababu hiyo nilinena; sisi nasi twaamini, na kwa sababu hiyo twanena; 14#1 Kor 6:14 tukijua ya kwamba yeye aliyemfufua Bwana Yesu atatufufua sisi nasi pamoja na Yesu, na kutuweka mbele yake pamoja nanyi. 15#2 Kor 1:3-6 Kwa maana mambo yote ni kwa ajili yenu, ili neema hiyo ikiongezwa sana, kwa hao walio wengi shukrani izidishwe, na Mungu atukuzwe.
Kuishi kwa imani
16 # Efe 3:16 Kwa hiyo hatulegei; bali ijapokuwa utu wetu wa nje unachakaa, lakini utu wetu wa ndani unafanywa upya siku kwa siku. 17#Rum 8:17,18 Maana dhiki yetu nyepesi, iliyo ya muda mfupi tu, yatuandalia utukufu wa milele uzidio kuwa mwingi sana; 18#Ebr 11:1,3; Kol 1:16 tusiviangalie vinavyoonekana, bali visivyoonekana. Kwa maana vinavyoonekana ni vya muda tu; bali visivyoonekana ni vya milele.

Iliyochaguliwa sasa

2 Wakorintho 4: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha