Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 Wakorintho 2

2
1 # 2 Kor 12:21; 1 Kor 4:21 Lakini nafsini mwangu nilikusudia hivi, nisije kwenu tena kwa huzuni. 2Maana mimi nikiwatia huzuni, basi ni nani anifurahishaye mimi ila yeye ahuzunishwaye nami? 3Nami niliwaandikia neno lilo hilo, ili nijapo nisitiwe huzuni na wale ambao ilinipasa kuwafurahia; nikiwatumaini ninyi nyote kwamba furaha yangu ni yenu nyote pia. 4#Mdo 20:31 Maana katika dhiki nyingi na taabu ya moyo niliwaandikia nikiwa na machozi mengi; si kwamba mhuzunishwe, bali mpate kujua upendo wangu nilio nao kwenu jinsi ulivyo mwingi.
Msamaha kwa mkosaji
5 # 1 Kor 5:1 Lakini iwapo mtu amehuzunisha, hakunihuzunisha mimi tu, bali kwa sehemu (nisije nikalemea mno), amewahuzunisha ninyi nyote. 6Yamtosha mtu wa namna hii adhabu ile aliyopewa na walio wengi; 7hata kinyume cha hayo, ni afadhali mmsamehe na kumfariji, mtu kama huyo asije akamezwa katika huzuni yake ipitayo kiasi. 8Kwa hiyo nawasihi kumthibitishia upendo wenu. 9#2 Kor 7:15 Maana niliandika kwa sababu hii pia, ili nipate wazi kwenu kwamba mmekuwa wenye kutii katika mambo yote. 10#Lk 10:16 Lakini kama mkimsamehe mtu neno lolote, nami nimemsamehe; kwa maana mimi nami, ikiwa nimemsamehe mtu neno lolote, nimemsamehe kwa ajili yenu mbele za Kristo, 11#Lk 22:31 Shetani asije akapata kutushinda; kwa maana hatukosi kuzijua fikira zake.
Wasiwasi wa Paulo huko Troa
12 # Mdo 20:1; 14:27; 1 Kor 16:9 Basi nilipofika Troa kwa ajili ya Injili ya Kristo, nikafunguliwa mlango katika Bwana, 13sikuona raha nafsini mwangu, kwa sababu sikumwona Tito ndugu yangu, bali niliagana nao, nikaondoka kwenda Makedonia. 14Ila Mungu ashukuriwe, anayetufanya tushangilie ushindi daima katika Kristo, na kuidhihirisha harufu ya kumjua yeye kila mahali kwa kazi yetu. 15#1 Kor 1:18 Kwa maana sisi tu manukato ya Kristo, mbele za Mungu, katika wao wanaookolewa, na katika wao wanaopotea; 16#2 Kor 3:5,6; Lk 2:34 katika hao wa pili harufu ya mauti iletayo mauti; katika hao wa kwanza harufu ya uzima iletayo uzima. Naye ni nani atoshaye kwa mambo hayo? 17#2 Kor 1:12; 1 Pet 4:11 Kwa maana sisi si kama walio wengi, walichuuzao neno la Mungu; bali kama kwa weupe wa moyo, kama kutoka kwa Mungu, mbele za Mungu, twanena katika Kristo.

Iliyochaguliwa sasa

2 Wakorintho 2: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha