Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Samweli 2:2-9

1 Samweli 2:2-9 SRUV

Hakuna aliye mtakatifu kama BWANA; Kwa maana hakuna yeyote ila wewe, Wala hakuna mwamba kama Mungu wetu. Msizidi kunena kwa kutakabari hivyo; Majivuno yasitoke vinywani mwenu; Kwa kuwa BWANA ni Mungu wa maarifa, Naye huyapima matendo kwa mizani. Pinde zao mashujaa zimevunjika, Na hao waliojikwaa wamepata nguvu. Walioshiba wamejikodisha ili kupata chakula, Lakini waliokuwa na njaa sasa hawana njaa tena. Naam, huyo aliyekuwa tasa amezaa watoto saba, lakini aliye na watoto wengi amehuzunika. BWANA huua, naye hufanya kuwa hai; Hushusha hadi kuzimu, tena huleta juu. BWANA hufukarisha mtu, na hutajirisha; Hushusha chini, tena huinua juu. Humwinua mnyonge kutoka mavumbini, Humpandisha mhitaji kutoka jaani, Ili awaketishe pamoja na wakuu, Wakakirithi kiti cha enzi cha utukufu; Kwa maana nguzo za dunia zina BWANA, Naye ameuweka ulimwengu juu yake. Yeye atailinda miguu ya watakatifu wake; Bali waovu watanyamazishwa gizani, Maana kwa nguvu hakuna atakayeshinda

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na 1 Samweli 2:2-9

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha