1 Samweli 15:32-33
1 Samweli 15:32-33 SRUV
Ndipo Samweli akasema, Nileteeni hapa Agagi, mfalme wa Waamaleki. Basi Agagi akamwendea kwa ulegevu. Naye Agagi akasema, Bila shaka uchungu wa mauti umeondoka. Lakini Samweli akamjibu, Kama upanga wako ulivyofanya wanawake kufiwa na watoto wao, vivyo hivyo mama yako atafiwa miongoni mwa wanawake. Basi Samweli akamkata Agagi vipande mbele za BWANA huko Gilgali.

