Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Petro 5

5
Kuchunga kundi la Mungu
1 # 2 Yoh 1:1; 3 Yoh 1:1; Rum 8:17; Ufu 1:9 Nawasihi wazee walio kwenu, mimi niliye mzee, mwenzi wao, na shahidi wa mateso ya Kristo, na mshirika wa utukufu utakaofunuliwa baadaye; 2#Yn 10:12; 21:15-17; Flm 1:14; Tit 1:11; Mdo 20:28; 1 Tim 3:2-7 lichungeni kundi la Mungu lililo kwenu, na kulisimamia, si kwa kulazimishwa, bali kwa hiari kama Mungu atakavyo; si kwa kutaka fedha ya aibu, bali kwa moyo. 3#2 Kor 1:24; Tit 2:7; Flp 3:17; 1 The 1:7 Wala si kama wajifanyao mabwana wa wale walio chini ya utunzaji wao, bali iweni mifano kwa lile kundi. 4#1 Pet 2:25; Ebr 13:20; 1 Kor 9:25; 2 Tim 4:8 Na Mchungaji mkuu atakapodhihirishwa, mtalipokea taji la utukufu, lile lisilokauka. 5#Mit 3:34; Efe 5:21; Mt 23:12; Yn 13:4,14; Yak 4:6 Vivyo hivyo ninyi vijana, watiini wazee. Naam, ninyi nyote jifungeni unyenyekevu, mpate kuhudumiana; kwa sababu Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema.
6 # Mt 23:12; Lk 14:11; 18:14; Ayu 22:29; Yak 4:10 Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake; 7#Zab 55:22; Mt 6:25; Flp 4:6 huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu. 8#1 The 5:6; Lk 18:3; Yak 4:7 Muwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka zunguka, akitafuta mtu ammeze. 9#Efe 6:11-13 Nanyi mpingeni huyo, mkiwa thabiti katika imani, mkijua ya kuwa mateso yale yale yanatimizwa kwa ndugu zenu kote duniani. 10#1 Pet 1:6; 1 The 2:12 Na Mungu wa neema yote, aliyewaita kuingia katika utukufu wake wa milele katika Kristo, mkiisha kuteswa kwa muda kidogo, yeye mwenyewe atawaimarisha, atawathibitisha, atawatia nguvu na kuwapa msingi imara. 11Uweza una yeye hata milele na milele. Amina.
Salamu za mwisho na baraka
12 # Mdo 15:22,40; Ebr 13:22 Kwa mkono wa Silwano, ndugu mwaminifu kama nijuavyo, nimewaandikia kwa maneno machache, kuonya na kushuhudia ya kuwa hii ndiyo neema ya kweli ya Mungu. Simameni imara katika hiyo. 13#Mdo 12:12,25; 13:13; 15:37-39; Kol 4:10; Flm 1:24; 2 Tim 4:11 Mwenzenu mteule hapa Babeli awasalimu, na Marko mwanangu. 14#1 Kor 16:20 Salimianeni kwa busu la upendo.
Amani na iwe kwenu nyote, mlio katika Kristo. Amina.

Iliyochaguliwa sasa

1 Petro 5: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha