Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Petro 1

1
Salamu
1 # Yak 1:1 Petro, mtume wa Yesu Kristo, kwa wateule wa Utawanyiko, wakaao hali ya ugeni katika Ponto, na Galatia, na Kapadokia, na Asia, na Bithinia; 2#Rum 8:29; Ebr 12:24 kama vile Mungu Baba alivyotangulia kuwajua katika kutakaswa na Roho, hata mkapata kutii na kunyunyiziwa damu ya Yesu Kristo. Neema na amani na ziongezwe kwenu.
Tumaini hai
3 # Yak 1:18 Ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa rehema zake nyingi alituzaa mara ya pili ili tupate tumaini lenye uzima kwa kufufuka kwake Yesu Kristo katika wafu; 4#Kol 1:12 tupate na urithi usioharibika, usio na uchafu, usionyauka, uliotunzwa mbinguni kwa ajili yenu. 5#Yn 10:28; 17:11; Rum 5:3,4; Gal 3:23; 1 Kor 2:5 Nanyi mnalindwa na nguvu za Mungu kwa njia ya imani ili mpate wokovu ulio tayari kufunuliwa wakati wa mwisho. 6#1 Pet 5:10; Ebr 12:11; Yak 1:2; 2 Kor 4:17 Mnafurahi sana wakati huo, ijapokuwa sasa kwa muda mfupi, ikiwa ni lazima, mmehuzunishwa kwa majaribu ya namna mbalimbali; 7#Mit 17:3; Mal 3:3; Rum 2:7,10; Yak 1:3 ili kwamba kujaribiwa kwa imani yenu, ambayo ina thamani kuu kuliko dhahabu ipoteayo, ijapokuwa hiyo hujaribiwa kwa moto, kuonekane kuwa kwenye sifa na utukufu na heshima, katika kufunuliwa kwake Yesu Kristo. 8#Yn 17:20; 20:29; 2 Kor 5:7; 2 Tim 4:8 Naye mwampenda, ijapokuwa hamkumwona; ambaye ijapokuwa hamumwoni sasa, mnamwamini; na kufurahi sana, kwa furaha isiyoneneka, yenye utukufu, 9#Rum 6:22 katika kuupokea mwisho wa imani yenu, yaani, wokovu wa roho zenu. 10#Mt 13:17; Lk 10:24 Kuhusu wokovu huo, manabii ambao walitabiri habari za neema itakayowafikia ninyi, walichunguza sana. 11#Zab 22:1; Isa 52:13—53:12; Lk 24:26 Wakatafuta ni wakati upi, na wakati wa namna gani ulioonywa na Roho wa Kristo aliyekuwa ndani yao, ambaye alitangulia kuyashuhudia mateso yatakayompata Kristo, na utukufu utakaokuwako baada ya hayo. 12#Efe 3:10; Lk 2:13 Wakafunuliwa ya kuwa si kwa ajili yao wenyewe, bali kwa ajili yenu walihudumu katika mambo hayo, ambayo sasa yamehubiriwa kwenu na wale waliowahubiria ninyi Injili kwa Roho Mtakatifu aliyetumwa kutoka mbinguni. Mambo hayo malaika wanatamani kuyaona.
Wito wa kuishi maisha ya utakatifu
13 # Lk 12:35; Efe 6:14 Kwa hiyo iweni tayari, na makini;#1:13 Kigiriki ni ‘Vifungeni viuno vya nia zenu na kuwa na kiasi’. mkiitumainia kwa utimilifu ile neema mtakayoletewa katika ufunuo wake Yesu Kristo. 14#Rum 12:2; Efe 2:3; 4:17 Kama watoto wa kutii msijifananishe na tamaa zenu za kwanza za ujinga wenu; 15bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote; 16#Law 11:44-45; 19:2; 20:7 kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu. 17#Zab 89:26; Yer 3:19; Mal 1:6; Mt 6:9; Rum 2:11 Na ikiwa mnamwita Baba, yeye ahukumuye kila mtu pasipo upendeleo, kwa kadiri ya kazi yake, nendeni kwa hofu katika wakati wenu wa kukaa hapa kama wageni. 18#Isa 52:3; 1 Kor 6:20; 7:23 Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu; mpate kutoka katika mwenendo wenu usiofaa mlioupokea kwa baba zenu; 19#Isa 53:7; Ebr 9:14 bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana-kondoo asiye na dosari wala waa, yaani, ya Kristo. 20#Rum 16:25; Efe 1:4 Naye amejulikana kweli tangu zamani, kabla haijawekwa misingi ya dunia; lakini alifunuliwa siku hizi za mwisho kwa ajili yenu; 21#Yn 14:6; Rum 4:24; Kol 1:27 na kupitia kwake mmekuwa wenye kumwamini Mungu, aliyemfufua katika wafu akampa utukufu; hata imani yenu na tumaini lenu liwe kwa Mungu. 22#1 Yoh 5:1 Mkiisha kujitakasa roho zenu kwa kuitii kweli, hata kuufikia upendano wa ndugu usio na unafiki, basi jitahidini kupendana kwa moyo safi. 23#Dan 6:26; Yn 1:13; Yak 1:18 Kwa kuwa mmezaliwa mara ya pili; si kwa mbegu iharibikayo, bali kwa ile isiyoharibika; kwa neno la Mungu lenye uzima, linalodumu hata milele. 24#Isa 40:6-8; Yak 1:10,11 Maana,
Mwili wote ni kama majani,
Na fahari yake yote ni kama ua la majani.
Majani hukauka na ua lake huanguka;
25 # Isa 40:8 Bali Neno la Bwana hudumu hata milele.
Na neno hilo ni neno lile jema lililohubiriwa kwenu.

Iliyochaguliwa sasa

1 Petro 1: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha