Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 92

92
Shukrani kwa ajili ya Uthibitisho
Zaburi. Wimbo wa Siku ya Sabato.
1Ni neno jema kumshukuru BWANA,
Na kuliimbia jina lako, Ee Uliye juu.
2Kuzitangaza rehema zako asubuhi,
Na uaminifu wako wakati wa usiku.
3Kwa chombo chenye nyuzi kumi,
Na kwa kinanda,
Na kwa mlio wa kinubi.
4Kwa kuwa umenifurahisha, BWANA,
Kwa kazi yako; nitashangilia
Kwa ajili ya matendo ya mikono yako.
5 # Isa 28:29; Rum 11:23 Ee BWANA, jinsi yalivyo makuu matendo yako!
Mawazo yako ni mafumbo makubwa.
6 # Zab 73:22 Mtu mjinga hayatambui hayo,
Wala mpumbavu hayafahamu.
7 # Ayu 21:7; Yer 12:1; Mal 3:15 Wasio haki wakichipuka kama majani
Na wote watendao maovu wakistawi.
Ni kwa kusudi waangamizwe milele;
8Bali Wewe, BWANA, U Mtukufu hata milele.
9Maana hao adui zako, Ee BWANA,
Hao adui zako watapotea,
Na watendao maovu watatawanyika wote pia.
10Bali pembe yangu umeiinua kama pembe ya nyati,
Nimepakwa mafuta mabichi.
11Na jicho langu limewatazama walioniotea,
Sikio langu limesikia habari za waovu walionishambulia.
12 # Zab 52:8; Wim 7:7 Mwenye haki atasitawi kama mtende,
Atakua kama mwerezi wa Lebanoni.
13 # Isa 60:21; Mt 15:13; Yn 15:2,5 Waliopandwa katika nyumba ya BWANA
Watasitawi katika nyua za Mungu wetu.
14Watazaa matunda hadi wakati wa uzee,
Watajaa utomvu, watakuwa na ubichi.
15 # Kum 32:4; Rum 9:14 Watangaze ya kuwa BWANA ni mwenye adili,
Mwamba wangu, ndani yake hamna udhalimu.

Iliyochaguliwa sasa

Zab 92: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha