Zab 89:15-17
Zab 89:15-17 SUV
Heri watu wale waijuao sauti ya shangwe, Ee BWANA, huenenda katika nuru ya uso wako. Kwa jina lako hufurahi mchana kutwa, Na kwa haki yako hutukuzwa. Maana fahari ya nguvu zao ni Wewe, Na kwa radhi yako pembe yetu itatukuka.