Zab 89:1-4
Zab 89:1-4 SUV
Fadhili za BWANA nitaziimba milele; Kwa kinywa changu nitavijulisha vizazi vyote uaminifu wako. Maana nimesema, Fadhili zitajengwa milele; Katika mbingu utauthibitisha uaminifu wako. Nimefanya agano na mteule wangu, Nimemuapia Daudi, mtumishi wangu. Wazao wako nitawafanya imara milele, Nitakijenga kiti chako cha enzi hata milele.