Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 89:1-11

Zab 89:1-11 SUV

Fadhili za BWANA nitaziimba milele; Kwa kinywa changu nitavijulisha vizazi vyote uaminifu wako. Maana nimesema, Fadhili zitajengwa milele; Katika mbingu utauthibitisha uaminifu wako. Nimefanya agano na mteule wangu, Nimemuapia Daudi, mtumishi wangu. Wazao wako nitawafanya imara milele, Nitakijenga kiti chako cha enzi hata milele. Ee BWANA, mbingu zitayasifu maajabu yako, Uaminifu wako katika kusanyiko la watakatifu. Maana ni nani katika mbingu awezaye kulinganishwa na BWANA? Ni nani afananaye na BWANA miongoni mwa malaika? Mungu huogopwa sana barazani pa watakatifu, Ni wa kuhofiwa kuliko wote wanaomzunguka. BWANA, Mungu wa majeshi, Ni nani aliye hodari kama Wewe, Ee YAHU? Na uaminifu wako unakuzunguka. Wewe ndiwe ukitawalaye kiburi cha bahari. Mawimbi yake yainukapo wayatuliza Wewe. Ndiwe uliyemseta Rahabu akawa kama aliyeuawa, Kwa mkono hodari umewatawanya wakuchukiao. Mbingu ni mali yako, nchi nayo ni mali yako, Ulimwengu na vyote viujazavyo Ndiwe uliyeupiga msingi wake.

Soma Zab 89

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Zab 89:1-11

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha