Zab 8:3-9
Zab 8:3-9 SUV
Nikiziangalia mbingu zako, kazi ya vidole vyako, Mwezi na nyota ulizoziratibisha; Mtu ni kitu gani hata umkumbuke, Na binadamu hata umwangalie? Umemfanya mdogo punde kuliko Mungu; Umemvika taji ya utukufu na heshima; Umemtawaza juu ya kazi za mikono yako; Umevitia vitu vyote chini ya miguu yake. Kondoo, na ng’ombe wote pia; Naam, na wanyama wa kondeni; Ndege wa angani, na samaki wa baharini; Na kila kipitacho njia za baharini. Wewe, MUNGU, Bwana wetu, Jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani mwote!