Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 74

74
Ombi la Kutaka Msaada Wakati wa Kushindwa
Utenzi wa Asafu.
1 # Zab 95:7; Yer 23:1; Eze 34:8,31; Lk 12:32 Ee Mungu, mbona umetutupa milele?
Kwa nini hasira yako inatoka moshi
Juu ya kondoo wa malisho yako?
2Ulikumbuke kusanyiko lako,
Ulilolinunua zamani.
Ulilolikomboa liwe kabila ya urithi wako,
Mlima Sayuni ulioufanya maskani yako.
3Upainulie miguu yako palipoharibika milele;
Adui ameufanya kila ubaya katika patakatifu.
4 # Dan 6:27 Watesi wako wamenguruma kati ya kusanyiko lako;
Wameweka bendera zao ziwe alama.
5Wanaonekana kama watu wainuao mashoka,
Waikate miti ya msituni.
6Na sasa nakishi yake yote pia
Wanaivunja-vunja kwa mashoka na nyundo.
7Wamepatia moto patakatifu pako;
Wamelinajisi kao la jina lako hata chini.
8 # Zab 83:4 Walisema mioyoni mwao,
Na tuwaangamize kabisa;
Mahali penye mikutano ya Mungu
Wamepachoma moto katika nchi pia.
9 # 1 Sam 3:1; Mik 3:6; Mt 16:4 Hatuzioni ishara zetu, wala sasa hakuna nabii,
Wala kwetu hakuna ajuaye, hata lini?
10Ee Mungu, mtesi atalaumu hata lini?
Adui alidharau jina lako hata milele?
11Mbona unaurudisha mkono wako,
Naam, mkono wako wa kuume,
Uutoe kifuani mwako,
Ukawaangamize kabisa.
12 # Zab 44:4 Lakini Mungu ni mfalme wangu tokea zamani,
Afanyaye mambo ya wokovu katikati ya nchi.
13 # Kut 14:21; Isa 51:9 Wewe umeipasua bahari kwa nguvu zako,
Umevivunja vichwa vya nyangumi juu ya maji.
14 # Kut 17:5,6; Hes 14:9; Hes 20:11; Ayu 41:1; Isa 11:16; Isa 27:1; Yos 3:13; Zab 72:9; Zab 104:26; Zab 105:41; Hab 3:9; Ufu 16:12 Wewe uliviseta vichwa vya lewiathani,
Awe chakula cha watu wa jangwani.
15Wewe ulitokeza chemchemi na kijito;
Wewe ulikausha mito yenye maji sikuzote.
16Mchana ni wako, usiku nao ni wako,
Ndiwe uliyeufanya mwanga na jua.
17 # Mdo 17:26 Wewe uliiweka mipaka yote ya dunia,
Kaskazi na kusi Wewe ulizitengeneza.
18 # Ufu 16:19 Ee BWANA, uyakumbuke hayo, adui amelaumu,
Na watu wapumbavu wamelidharau jina lako.
19 # Wim 2:14; 4:1 Usimpe mnyama mkali nafsi ya hua wako;
Usiusahau milele uhai wa watu wako walioonewa.
20 # Mwa 17:7; Law 26:44; Yer 33:21 Ulitafakari agano;
Maana mahali penye giza katika nchi
Pamejaa makao ya ukatili.
21 # Zab 9:18 Aliyeonewa asirejee ametiwa haya,
Mnyonge na mhitaji na walisifu jina lako.
22 # Isa 37:23 Ee Mungu, usimame, ujitetee mwenyewe,
Ukumbuke unavyotukanwa na mpumbavu mchana kutwa.
23Usiisahau sauti ya watesi wako,
Ghasia yao wanaokuondokea inapaa daima.

Iliyochaguliwa sasa

Zab 74: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha