Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 73

73
KITABU CHA TATU
Ombi la kuponywa kutoka kwa Waonevu
Zaburi ya Asafu
1Hakika Mungu ni mwema kwa Israeli,
Kwa hao walio safi mioyo yao.
2Nami miguu yangu ilikuwa karibu na kupotoka,
Hatua zangu zilikuwa karibu na kuteleza.
3Maana naliwaonea wivu wenye kujivuna,
Nilipoiona hali ya amani ya wasio haki.
4Maana hawana maumivu katika kufa kwao,
Na mwili wao una nguvu.
5Katika taabu ya watu hawamo,
Wala hawapati mapigo pamoja na wanadamu.
6 # Mhu 8:11 Hivyo kiburi kimekuwa mkufu shingoni mwao,
Jeuri huwavika kama nguo.
7Macho yao hutokeza kwa kunenepa,
Wameipita kadiri ya mawazo ya mioyo yao.
8 # 2 Pet 2:18; Yud 1:16 Hudhihaki, husimulia mabaya,
Husimulia udhalimu kana kwamba wako juu.
9 # Ufu 13:6 Wameweka kinywa chao mbinguni,
Na ulimi wao hutanga-tanga duniani.
10Kwa hiyo watu wake hugeuka huko,
Na maji yaliyojaa humezwa nao.
11 # Ayu 22:13; Zab 94:7 Nao husema, Mungu ajuaje?
Yako maarifa kwake aliye juu?
12Fahamu, ndivyo walivyo wasio haki,
Na kwa kustarehe sikuzote wamepata mali nyingi.
13 # Ayu 21:15; Zab 24:4; Mal 3:14; Ebr 10:19-22 Hakika nimejisafisha moyo wangu bure,
Nimenawa mikono yangu kwa kutokukosa.
14Maana mchana kutwa nimepigwa,
Na kuadhibiwa kila asubuhi.
15Kama ningalisema, Nitasimulia kama hayo;
Kumbe! Ningaliwadanganya kizazi cha wana wako.
16 # Mhu 8:17 Nami nalifikiri jinsi ya kufahamu hayo;
Ikawa taabu machoni pangu;
17 # Zab 77:13 Hata nilipoingia katika patakatifu pa Mungu,
Nikautafakari mwisho wao.
18Hakika Wewe huwaweka penye utelezi,
Huwaangusha mpaka palipoharibika.
19Namna gani wamekuwa ukiwa mara!
Wametokomea na kutoweshwa kwa utisho.
20Ee Bwana, kama ndoto wakati wa kuamka,
Uondokapo utaidharau sanamu yao.
21Moyo wangu ulipoona uchungu,
Viuno vyangu viliponichoma,
22Nalikuwa kama mjinga, sijui neno;
Nalikuwa kama mnyama tu mbele zako.
23Walakini mimi ni pamoja nawe daima,
Umenishika mkono wa kuume.
24 # Isa 58:8; Yn 14:3; 2 Kor 5:1 Utaniongoza kwa shauri lako,
Na baadaye utanikaribisha kwa utukufu.
25 # Isa 26:8,9; Hab 3:17,18 Ni nani niliye naye mbinguni,
Wala duniani sina cha kupendeza ila Wewe.
26 # Zab 84:2 Mwili wangu na moyo wangu hupunguka,
Bali Mungu ni mwamba wa moyo wangu
Na sehemu yangu milele.
27Maana wajitengao nawe watapotea;
Umewaangamiza wote waliokuacha Wewe.
28 # Ebr 10:22 Nami kumkaribia Mungu ni kwema kwangu;
Nimefanya kimbilio kwa Bwana MUNGU,
Niyahubiri matendo yako yote.

Iliyochaguliwa sasa

Zab 73: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha