Zab 63:2-5
Zab 63:2-5 SUV
Ndivyo nilivyokutazama katika patakatifu, Nizione nguvu zako na utukufu wako. Maana fadhili zako ni njema kuliko uhai; Midomo yangu itakusifu. Ndivyo nitakavyokubariki maadamu ni hai; Kwa jina lako nitaiinua mikono yangu. Nafsi yangu itakinai kama kushiba mafuta na vinono; Kinywa changu kitakusifu kwa midomo ya furaha.