Zab 50:10-15
Zab 50:10-15 SUV
Maana kila hayawani ni wangu, Na makundi juu ya milima elfu. Nawajua ndege wote wa milima, Na wanyama wote wa mashamba ni wangu Kama ningekuwa na njaa singekuambia, Maana ulimwengu ni wangu, navyo viujazavyo. Je! Nile nyama ya mafahali! Au ninywe damu ya mbuzi! Mtolee Mungu dhabihu za kushukuru; Mtimizie Aliye juu nadhiri zako. Ukaniite siku ya mateso; Nitakuokoa, na wewe utanitukuza.