Zab 35:12-14
Zab 35:12-14 SUV
Wananilipa mabaya badala ya mema, Hata nafsi yangu ikaingia ukiwa. Bali mimi, walipougua wao, Nguo yangu ilikuwa gunia. Nalijitesa nafsi yangu kwa kufunga; Maombi yangu yakarejea kifuani mwangu. Nalijifanya kama kwamba ni rafiki au ndugu yangu, Naliinama nikilia kama aliyefiwa na mamaye.