Zab 34:15-18
Zab 34:15-18 SUV
Macho ya BWANA huwaelekea wenye haki, Na masikio yake hukielekea kilio chao. Uso wa BWANA ni juu ya watenda mabaya, Aliondoe kumbukumbu lao duniani. Walilia, naye BWANA akasikia, Akawaponya na taabu zao zote. BWANA yu karibu nao waliovunjika moyo, Na waliopondeka roho huwaokoa.