Zab 33:6-9
Zab 33:6-9 SUV
Kwa neno la BWANA mbingu zilifanyika, Na jeshi lake lote kwa pumzi ya kinywa chake. Hukusanya maji ya bahari chungu chungu, Huviweka vilindi katika ghala. Nchi yote na imwogope BWANA, Wote wakaao duniani na wamche. Maana Yeye alisema, ikawa; Na Yeye aliamuru, ikasimama.