Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 30

30
Shukrani kwa Kuponywa Maradhi Mabaya
Zaburi. Wimbo wa kuweka wakfu hekalu. Ya Daudi.
1Ee BWANA, nitakutukuza kwa maana umeniinua,
Wala hukuwafurahisha adui zangu juu yangu.
2 # Zab 6:2-4 Ee BWANA, Mungu wangu,
Nalikulilia ukaniponya.
3 # Zab 40:1,2 Umeniinua nafsi yangu,
Ee BWANA, kutoka kuzimu.
Umenihuisha na kunitoa
Miongoni mwao washukao shimoni.
4Mwimbieni BWANA zaburi,
Enyi watauwa wake.
Na kufanya shukrani.
Kwa kumbukumbu la utakatifu wake.
5 # Zab 16:11; Ufu 22:17 Maana ghadhabu zake ni za kitambo kidogo,
Katika radhi yake mna uhai.
Huenda kilio huja kukaa usiku,
Lakini asubuhi huwa furaha.
6 # Ayu 29:18 Nami nilipofanikiwa nalisema,
Sitaondoshwa milele.
7 # Zab 104:29 BWANA, kwa radhi yako
Wewe uliuimarisha mlima wangu.
Uliuficha uso wako,
Nami nikafadhaika.
8Ee BWANA, nalikulilia Wewe,
Naam, kwa BWANA naliomba dua.
9 # Zab 115:17 Mna faida gani katika damu yangu
Nishukapo shimoni?
Mavumbi yatakusifu?
Yataitangaza kweli yako?
10 # Zab 4:1 Ee BWANA, usikie, unirehemu,
BWANA, uwe msaidizi wangu.
11 # 2 Sam 6:14 Uligeuza matanga yangu kuwa machezo;
Ulinivua gunia, ukanivika furaha.
12Ili utukufu wangu ukusifu,
Wala usinyamaze.
Ee BWANA, Mungu wangu,
Nitakushukuru milele.

Iliyochaguliwa sasa

Zab 30: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha