Zab 28:6-9
Zab 28:6-9 SUV
Na ahimidiwe BWANA. Maana ameisikia sauti ya dua yangu; BWANA ni nguvu zangu na ngao yangu. Moyo wangu umemtumaini, Nami nimesaidiwa; Basi, moyo wangu unashangilia, Na kwa wimbo wangu nitamshukuru. BWANA ni nguvu za watu wake, Naye ni ngome ya wokovu kwa masihi wake. Uwaokoe watu wako, uubariki urithi wako, Uwachunge, uwachukue milele.