Zab 27:6-9
Zab 27:6-9 SUV
Na sasa kichwa changu kitainuka Juu ya adui zangu wanaonizunguka. Nami nitatoa dhabihu za shangwe hemani mwake; Nitaimba, naam, nitamhimidi BWANA. Ee BWANA, usikie, kwa sauti yangu ninalia, Unifadhili, unijibu. Uliposema, Nitafuteni uso wangu, Moyo wangu umekuambia, BWANA, uso wako nitautafuta. Usinifiche uso wako, Usijiepushe na mtumishi wako kwa hasira. Umekuwa msaada wangu, usinitupe, Wala usiniache, Ee Mungu wa wokovu wangu.