Zab 25:4-7
Zab 25:4-7 SUV
Ee BWANA, unijulishe njia zako, Unifundishe mapito yako, Uniongoze katika kweli yako, Na kunifundisha. Maana Wewe ndiwe Mungu wa wokovu wangu, Nakungoja Wewe mchana kutwa. Ee BWANA, kumbuka rehema zako na fadhili zako, Maana zimekuwako tokea zamani. Usiyakumbuke makosa ya ujana wangu, Wala maasi yangu. Unikumbuke kwa kadiri ya fadhili zako, Ee BWANA kwa ajili ya wema wako.